SOMA ALICHOKISEMA MKE WAKE HAPA
Soka ni mchezo wenye mashabiki wengi sana duniani na kuna wengine wako tayari kufanya usivyoweza kutegemea, hata kujitoa uhai.AFANDE SELE.
JUMAMOSI (May 18) kulikuwa na mpambano wa watani wajadi Simba na Yanga na timu ya Simba iliupoteza mchezo huo kwa kufungwa magoli 2 kwa bila na Yanga.
King Selemani ama Afande Sele kutoka mji kasoro bahari Morogoro ni moja ya watu wanaoonekana kuwa ‘addicted’ na ushabiki wa soka kiasi cha kushind
wa kuvumilia maumivu ya kufungwa kwa timu anayoishabikia, Simba kitendo kilichompelekea asuse kula toka Jumamosi.
Akizungumza na Suddy Brown katika segment maarufu ya U Heard kupitia XXL ya Clouds FM, mke wa rapper huyo mkongwe Mama Tunda, amethibitisha kuwa mumewe amegoma kula toka siku ya mechi.
Mbaya zaidi kwa Afande ni kuwa Mama Tunda na binti yao Tunda ni mashabiki wa Yanga hivyo wao na Selemani Msindi ni mashabiki wa timu mbili pinzani, hatupati picha humo ndani panavyokuwa ikifungwa timu anayoshabikia baba wa familia!.
Minuno ya hatari bila shaka. Pole Afande.
CHANZO : BONGO5
0 comments:
Post a Comment