MWANANCHI
DASPIKA wa Bunge, Anne Makinda jana aliizima hoja ya Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuhusu umiliki wa mashamba makubwa yasiyoendelezwa wakati wa kujadili hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambayo ilihitimishwa bungeni jana.
Mdee alivutana na Spika Makinda wakati wa kujadili
bajeti hiyo kifungu kwa kifungu, Mdee alipot
aka kufahamu kauli ya Serikali kuhusu kampuni zinazomiliki ardhi bila kuziendeleza na hatua zinazochukua kuhakikisha zinarudishwa kwa wananchi.
aka kufahamu kauli ya Serikali kuhusu kampuni zinazomiliki ardhi bila kuziendeleza na hatua zinazochukua kuhakikisha zinarudishwa kwa wananchi.
Baada ya kuuliza swali hilo huku akisisitiza kutoa
shilingi, Spika Makinda alimtaka kukaa chini kwa kuwa hoja yake haina
mashiko ya kufanya hivyo na kwamba kama anataka aiwasilishe kama hoja
binafsi.
“Kaa chini, nakwambia kaa chini,” alisema Makinda
huku Mdee akionekana kuendelea kuzungumza... “Nasema kaa chini,”
alirudia na Mdee kukaa huku akikipeperusha karatasi hewani kuonyesha
kutokubaliana naye.
Awali, Mdee alisema shamba la Simanjiro ambalo
Halmashauri ya wilaya hiyo ilipendekeza mwekezaji kupewa ekari 500
lakini Wizara ya Ardhi iliidhinisha ekari 25,000 ambazo mwekezaji
hajaziendeleza zote wakati mashamba ya Kisarawe na mashamba ya mkonge
Tanga ambayo wawekezaji wameyakopea fedha nayo hadi sasa
hayajaendelezwa.
Alitaka kauli ya Serikali kuhusiana na hali hiyo
na jinsi ya kurudisha mashamba hayo katika miliki ya umma. Mbunge
mwingine aliyetishia kutoa shilingi ni Dk Faustine Ndungulile wa
Kigamboni (CCM), akijikita katika suala la ujenzi wa mji mpya wa
Kigamboni akisema wananchi wake hawakushirikishwa katika mipango ya
ujenzi huo.
Akijibu hoja hizo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema wananchi
wameshirikishwa kikamilifu katika mchakato mzima na kuahidi kukaa na
mbunge huyo pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema
kuzungumzia suala la Kigamboni.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Goodluck ole Medeye alisema kila mkazi atalipwa Sh35,000 kwa
kila mita moja ya mraba na mwenye ekari moja atapata Sh141 milioni na
kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwa mradi huo utakuwa wa
maendeleo kwa kila mmoja.
Baada ya majibu hayo, Dk Ndungulile alisimama na
kusema kuwa anakubali kurejesha shilingi hasa baada ya Waziri Tibaijuka
kutamka kuwa wananchi wameshirikishwa na watashirikishwa katika kutatua
mgogoro wa Kigamboni.
Spika Makinda aliwataka kushirikiana kutatua mgogoro wa Kigamboni ili mradi uanze.
0 comments:
Post a Comment