MTANZANIA.
SIKU moja baada ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel
Sitta kutangaza timu inayoundwa na kundi lake kuwania ukuu wa dola mwaka
20
15, maswali yameibuka kuhusu uadilifu wa timu hiyo.
Juzi wakati akizungumza katika kongamano la Mawasiliano katika Nyanja ya
Digitali la wanafunzi wa idara ya uhusiano na Masoko wa Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustine (SAUT) jijini Mwanza, Sitta aliitaja timu hiyo
inayoundwa na watu wanne kuwa mmoja wao atawania urais katika uchaguzi
mkuu ujao mwaka 2015.
Alisema wanaounda timu hiyo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli na Waziri wa
Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe.
Kutajwa kwa vigogo hao kumeibua maswali toka kwa wachambuzi na
wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa nchini, ambao wamechambua wasifu wa
kila mmoja ikiwa ni pamoja na kupima utendaji na uadilifu wao kama
wanafaa kupewa dhamana ya kuongoza nchi.
Sitta
Sitta ambaye kabla ya kuwa Waziri wa Afrika
Mashariki, aliwahi kuwa Spika wa Bunge, baadhi ya wachambuzi
wanamuelezea kuwa ni mwanasiasa mlafi wa madaraka, udhaifu ambao
ulimsababishia afarakane na baadhi ya wanasiasa wenzake ndani ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Watu wanaomfahamu Sitta, wanadai kuwa
udhaifu wake huo ndio uliomtuma ashiriki siasa chafu ambazo kwa kiasi
kikubwa zilisababisha kukiathiri chama.
Sitta kwa kushirikiana na
Dk. Mwakyembe, wanadaiwa kushiriki kuiua CCM kutokana na kutajwa kuwa
nyuma ya mpango wa kuanzisha chama kingine cha siasa, Chama cha Jamii
(CCJ), wakiwa bado CCM.
Inadaiwa kuwa uroho wa madaraka
ulimsukuma Sitta kushiriki kuuaminisha umma alikuwa akipambana kuibadili
CCM kutoka kwenye makucha ya matajiri na mafisadi wachache,
akijipambanua kuwa ni mpambanaji wa ufisadi.
Ni katika msingi huo
huo Spika Sitta aliunda Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk.
Mwakyembe kuchunguza uhalali wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond,
ambayo ilimuondoa madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.
Sitta
akishirikiana na baadhi ya wanasiasa akiwemo Dk. Mwakyembe
wanashutumiwa kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha ukuaji wa
uchumi nchini, kutokana na hatua ya kushinikiza kutonunuliwa mitambo ya
Dowans iliyorithi mkataba wa kampuni ya Richmond kwa madai kuwa ni ya
kifisadi.
Ni tabia hiyo ya usaliti ya Sitta ndiyo inayoelezwa
kuchagiza harakati zilizoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, kumuondoa
katika wadhifa wa uspika na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa naibu
wake Anne Makinda.
Wanaoamini hivyo, wanarejea taarifa zilizopata
kuvuma pasipo yeye mwenyewe kuzitolea maelezo za kusudio lake la kutaka
kujiunga na Chadema ili apate madaraka baada ya kufarakana na waliokuwa
maswahiba wake wa kisiasa ndani ya CCM.
Wachambuzi wa masuala ya
kisiasa wanadai kuwa baada ya kupima upepo wa kisiasa, Sitta alisitisha
uamuzi huo wa kuhamia Chadema kabla chama chake hakijampooza na kumpa
uwaziri, baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.
Akiwa Spika, Sitta pia
aliwahi kukumbwa na kashfa ya ujenzi wa chini ya kiwango wa ukumbi wa
Bunge jipya, bunge hilo lililojengwa kwa mabilioni ya fedha lakini sasa
linavuja na ukaguzi umeonyesha kuwa halikujengwa kwa kiwango stahiki na
hakuna mitambo ya usalama iliyofungwa ukumbini humo na wakati huo huo
kupoteza nyaraka za jengo hilo ya michoro yake.
Ofisi ya Mbunge
Wanaompima Sitta kama anaweza
kuongoza nchi, pia wanaliangalia Jimbo lake la Urambo aliloliongoza kwa
takribani miaka 35, ambalo hadi leo linadaiwa kuwa liko nyuma
kimaendeleo.
Ni kwa muktadha huo, baadhi ya wachambuzi wanahoji
kama alishindwa kuliongoza jimbo lenye watu wachache na kulivusha kwenye
maendeleo, je ataweza kuongoza nchi yenye watu zaidi ya milioni 40?
Pamoja
na hilo pia anadaiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi
ndogo ya Spika, ambayo yeye aliita ya Mbunge jimboni humo.
Ingawa
Serikali iliridhia ofisi za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha
kisichozidi Sh milioni 40 kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi
hiyo ya Sitta jimboni Urambo, ilijengwa kwa Sh Milioni 350.
Wakati
huo huo alikuwa akidaiwa kujitibu kwa gharama ya shilingi milioni mbili
kwa kununua dawa za mamilioni ya fedha ili kutibu mguu, alizonunua
katika moja ya duka la dawa jijini Dar es Salaam.
Matumizi holela ya nyumba za Serikali
Sitta ni
mmoja wa vigogo waliopatiwa nyumba za Serikali, wakati watumishi wengine
wa Serikali wakikosa makazi na kuishi hotelini kwa gharama kubwa,
zinazolipwa na Serikali, Sitta ameendelea kuitumia nyumba hiyo kiholela
kwa kuweka biashara ya pombe.
Dk. Mwakyembe
Usaliti CCM
Kama ilivyo kwa Sitta,
wafuatiliaji wa siasa za hapa nchini pia wanatilia shaka uadilifu wa Dk.
Mwakyembe, kwa sababu ya uswahiba wake na Sitta na kubeba hoja
zinazofanana.
Chanzo uchumi kudorora
Dk. Mwakyembe ambaye ni Msomi na
Mwanasheria nguli, wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge ya
kuchunguza sakata la Richmond, anadaiwa kuwa alishiriki kuiaminisha
uongo Serikali na umma wa Watanzania kuhusu kampuni ya Richmond.
Akiwa
Mwenyekiti wa kamati hiyo teule, Dk. Mwakyembe na kamati yake walitoa
maazimio 23 ambayo Bunge liliitaka Serikali iyatekeleze, hadi sasa ni
maazimio 10 tu yameshafanyiwa kazi huku mengine 13 yakiwa bado hewani na
yasiyozungumziwa hata na yeye mwenyewe.
Hata hivyo Dk.
Mwakyembe anadaiwa kuipinga kampuni ya Dowans kwa sababu ya maslahi
yake, kutokana na kile kinachodaiwa kuwa kampuni hiyo ilikuwa ni
mshindani wa kampuni ambayo anadaiwa kuwa mmoja wa wamiliki wake ya
kufua umeme.
Dk. Mwakyembe ilibainika kuwa ni miongoni mwa watu
tisa wenye hisa katika kampuni binafsi ya kufua umeme wa kutumia nguvu
za upepo ya Power Pool East Africa Ltd, ambapo yeye anamiliki hisa 1,485
katika kampuni hiyo.
Kampuni hiyo tayari imeshapata maeneo ya kuwekeza katika maeneo ya Makambako mkoani Iringa na Singida.
Maeneo
hayo yanadaiwa kuwa na upepo mkali ambao ndiyo malighafi muhimu, hivyo
ujasiri wa Dk. Mwakyembe katika kuishambulia kampuni ya Richmond na
Dowans, unatokana na mgongano wa kimaslahi.
Ufisadi
Kashfa nyingine inayomkabili ni ya ujenzi wa bandari
ya nchi kavu kwa kampuni inayomilikiwa na CCM, kinyume cha sheria za
manunuzi.
Kampuni hiyo ya Jitegemee Trading Company, ilipewa
zabuni ya ujenzi wa bandari katika Viwanja vya Sukita bila kuwa na
mchakato wa kushindanisha kampuni nyingine.
Bernard Membe
Urais wa maadui
Wafuatiliaji wa masuala
ya kisiasa pia wameuchambua udhaifu wa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakisema kuwa hana uvumilivu
baada ya kudhihirisha udhaifu wake kuwa anao maadui 11, kati yao wawili
wakiwa ni waandishi wa habari ambao alidai pindi atakapokuwa Rais
atawashughulikia.
Kupigiwa debe na familia ya JK
Membe pia anatajwa kuwa
dhaifu kutokana na kushindwa kusimama yeye mwenyewe kisiasa na hivyo
kutegemea msaada wa familia ya rais Kikwete.
Wanaouelezea udhaifu
wa aina hiyo wa Membe wanakumbuka jinsi mwanasiasa huyo alivyopigiwa
kampeni ya ujumbe wa NEC na mke na mtoto wa Rais, hali inayowalazimu
watu kuamini kuwa Membe hana uwezo wa kujiamini.
Ikumbukwe kuwa Membe alishatangaza nia ya kugombea urais mwaka 2015 kwa kivuli cha kuombwa na wananchi kufanya hivyo.
Kashfa ya Ufisadi fedha za Libya
Ingawa Rais anapaswa kuwa
mwadilifu na muwajibikaji, Membe anatajwa kuwa alipewa fedha za nchi
huko Comoro, Morocco na Libya, lakini akazitia mfukoni.
Ilidaiwa
kuwa Waziri huyo alizitumia fedha hizo kwa ujenzi wa hoteli kubwa katika
makao makuu ya moja ya mikoa ya Kusini mwa Tanzania.
Fedha hizo
za mkopo dola za Marekani milioni 20, zilitolewa na Serikali ya Libya
wakati wa utawala wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Hayati Muamar Gaddafi.
Pamoja na kudai kuwa fedha hizo zilipaswa kupewa kampuni moja
ya Meize, kwa ajili ya kujenga kiwanda cha saruji mkoani Lindi, Membe
aliendelea kujikanganya na kudai kuwa kampuni ya Mohamed Enterprises
ilikuwa inashirikiana na ofisa mmoja wa ubalozi wa Libya ili apate fedha
hizo ambazo mpaka sasa zimeendelea kubaki kuwa kitendawili.
Dk. John Magufuli
Ufisadi
Kwa upande wake Dk. John
Magufuli ambaye ni Waziri wa Ujenzi, naye uadilifu wake kama kiongozi
unatiliwa shaka kutokana na kukumbwa na kashfa ya upotevu wa shilingi
252,975,000,000 zilizolipwa kwa mradi hewa, ambapo kiasi hicho cha fedha
kinadaiwa kuwa kingeweza kujenga barabara ya lami yenye urefu wa
kilomita 316.218.
Uamuzi wa kukurupuka
Baadhi ya maamuzi mengine ya Dk.
Magufuli yamelitumbukiza taifa katika hasara kubwa kama lile la kesi ya
uvuvi haramu, ambapo taifa lililazimika kulipa mabilioni ya fedha kama
gharama za kuhifadhi samaki hao wakati kesi hiyo ikiwa mahakamani.
Kama
kiongozi ambaye anatakiwa kusikiliza ushauri na kufuatilia kero na
malalamiko ya anaowaongoza, Dk. Magufuli amekuwa mzito ambapo watumishi
wa wizara yake wanamtaja kama mtu asiyeshaurika.
Uamuzi mwingine
wenye utata ambao uliligharimu taifa ni kuhusu suala la kuuza nyumba za
Serikali, ambalo hadi leo taifa linaujutia, upo ukweli kuwa alihusika
kugawa nyumba hizo hadi kwa ‘vimada’ wake, jambo ambalo linatiliwa shaka
uadilifu wake kiuongozi.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment