Kwa ufupi
Fedha hizo zilitakiwa kutumika kununulia malighafi,
vyombo vya usafiri wa barabara, vifaa vya kilimo na ujenzi, wakati huo
hali ya uchumi hususan ya upatikanaji wa fedha za kigeni ilikuwa mbaya,
hivyo mpango huu ulikuwa usaidie kuinusuru hali hiyo.http://www.mwananchi.co.tz
Hata mimi sina uhakika wa suala hilo, lakini kwa kumbukumbu nilizonazo, tulimalizana na hao watu siku nyingi sana.
Kimbisa
DAR ES SALAAM.
BAADHI ya wanasiasa, wafanyabiashara na wizara kadhaa za Serikali za Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wameendelea kukalia mabilioni ya shilingi waliyokopa kupitia uliokuwa Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa kutoka nje ya Nchi (Commodity Import Support - CIS).
Taarifa ambazo zimelifikia Mwananchi zinasema
kiasi cha fedha ambacho bado hakijarejeshwa na wakopaji hao ni Sh216
bilioni ambazo kama zingepatikana, zingetosha kugharimia madawati
milioni 2.7 kwa gharama ya Sh80,000 kila moja yenye uwezo wa kutosheleza
wanafunzi milioni 8.1.
CIS ni mpango ulioanzishwa na Serikali miaka ya
1980 na kuendelea hadi mwanzoni mwa mia
ka 2000, ambao nchi wahisani zikiongozwa na Japan zilikuwa zikiipatia Serikali fedha za kigeni ili kuimarisha sekta za biashara.
ka 2000, ambao nchi wahisani zikiongozwa na Japan zilikuwa zikiipatia Serikali fedha za kigeni ili kuimarisha sekta za biashara.
Nchi nyingine zilizochangia fedha hizo ni
Uingereza, Uholanzi, Saudi Arabia, Norway, Uswisi, Ubelgiji, Sweden na
Denmark na madeni yaliyotokana na fedha hizo ni sehemu ya deni la taifa
ambalo linagharimiwa na fedha za walipakodi wa sasa.
Hata hivyo, taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa
mpango huo ni kama ulihujumiwa na baadhi ya waliochota fedha hizo kwani
walizitumia kinyume cha makusudio na sasa ni kama Serikali imeshindwa
kuzirejesha licha ya kumwajiri mkusanyaji kwa mwaka mzima.
Fedha hizo zilitakiwa kutumika kununulia
malighafi, vyombo vya usafiri wa barabara, vifaa vya kilimo na ujenzi,
wakati huo hali ya uchumi hususan ya upatikanaji wa fedha za kigeni
ilikuwa mbaya, hivyo mpango huu ulikuwa usaidie kuinusuru hali hiyo.
Mwanzoni mwa 2011, Serikali iliingia mkataba wa
mwaka mmoja na kampuni ya udalali ya Msolopa Investiment Limited ambayo
kwa mujibu wa taarifa za uhakika, mkataba wake ulimalizika Januari mwaka
jana bila kutimiza lengo la kurejesha mabilioni hayo.
Mkataba huo ulifikia ukomo huku Msolopa ikiwa
imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh5 bilioni, sawa na asilimia 2.31 tu ya
Sh216 bilioni ambazo bado zinadaiwa mikononi mwa wakopaji.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msolopa, Ibrahim Msolopa alikataa kuzungumzia suala hilo akisema hana mamlaka...
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msolopa, Ibrahim Msolopa alikataa kuzungumzia suala hilo akisema hana mamlaka...
“Mkataba wangu na Serikali juu ya suala hilo
ulishafikia ukomo, nimeshakabidhi kila kitu kinachohusu CIS kwa Serikali
kwa hiyo kama mnahitaji taarifa yoyote nendeni serikalini.”
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema halifahamu suala la watu kudaiwa fedha za CIS... “Ninahitaji muda wa kulifuatilia suala hili na kufahamu undani wake.”
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema halifahamu suala la watu kudaiwa fedha za CIS... “Ninahitaji muda wa kulifuatilia suala hili na kufahamu undani wake.”
Vigogo wanaodaiwa
Uchunguzi umebaini kuwa fedha hizo zimekaliwa na wafanyabiashara na wanasiasa kupitia kampuni zao wakiwamo wabunge wa CCM, Abbas Mtemvu (Temeke) na Henry Shekifu (Lushoto), Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Ramadhan Madabida (Dar es Salaam) na Adam Kimbisa (Dodoma).

Kampuni ya Shamshi & Sons ya Shekifu ilikopa
Yen za Kijapani 12,778,082.81 (sawa na Sh.207 milioni) kwa kuzingatia
viwango vya sasa vya kubadilisha fedha ambavyo ni wastani wa Sh16.20
dhidi ya Yen moja.
Kampuni ya Cargo Plan International, ambayo
mmiliki wake ni Kimbisa ilikopa Yen 2,882,961.79 (zaidi ya Sh46.7
milioni), wakati Tanzania Pharmaceutical inayomilikiwa na Madabida
ilikopa Yen 7,031,983.29 (takriban Sh114 milioni).
0 comments:
Post a Comment