BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JESHI LA POLISI LAUA WATU 31 MWAKA 2012 TOFAUT NA MIAKA YA MINGINE.

CHANZO http://www.mtanzania.co.tz.Inspekta jenerali wa Polisi ,Said Mwema.

JUMLA ya watu 31 wameuawa na askari wa Jeshi la Polisi katika matukio mbalimbali yaliyotokea mwaka jana ukilinganisha na miaka ya nyuma. 

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na Askofu mstaafu, Elinaza Sendoro, katika uzinduzi wa taarifa ya Haki za Binadamu ya mwaka 2012 ya Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema pia pamoja na polisi kuuawa pia katika ripoti hiyo inaonyesha jumla ya askari tisa walivyouawa, vitendo vya ubakaji na kuingiliwa kinyume na maumbile watoto vitendo vinaonyesha ni ukiukwaji wa haki za binad

amu.

“Jamani hali hii inatisha tunaomba LHRC isaidie kwani Taifa hili linaelekea pabaya kwa kuwa watu wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi kitu ambacho ni hatari kwa Taifa linalokua kama hili.

“Tunahitaji nyie wanaharakati wa haki za binadamu mtutetee kwani hata vitabu vya dini zote vinapinga hali hii lakini nashangaa ni kwanini watoto, walemavu, wazee wanaonewa kiasi hiki,” alisema Sendoro.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa LHRC Harold Sungusia, alisema katika ripoti hii pia imeelezea ni jinsi gani waandishi wa habari wanavyonyanyaswa na kuuawa wakati wakiwa katika majukumu yao.

Alisema katika ripoti hiyo wamependekeza vipengele mbalimbali vinavyohusiana na haki za binadamu kuainishwa katika Katiba mpya inayotarajiwa kupatikana siku za karibuni.

“Tunataka kila Mtanzania ajivunie nchi yake na aishi kwa amani na upendo kwa kuwa matukio kama udharilishwaji wa watoto, kuteswa kwa wanahabari na kukosekana kwa haki mahakamani vikomeshwe,” alisema Sungusia.

Kuhusu usafirishwaji haramu wa binadamu, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku, Lutgard Kokulinda, alisema sheria inatakiwa kufanya kazi yake kwa kuwa watoto wamekuwa wakipelekwa katika mashamba ya tumbaku kufanyishwa kazi ngumu.

“Watoto hawana ulinzi wa kutosha kwa kuwa wamekuwa wakichukuliwa kwenda kufanya kazi katika mashamba ya tumbaku kule Urambo Tabora na hulipwa ujira mdogo na hukatishwa masomo yao,” alisema Kokulinda.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: