MWANANCHI. Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) wakiwa kwenye doria
HALI ya uhasama imeibuka kati ya polisi na raia mkoani Mtwara,
kila upande ukilalamika kuhujumiwa huku hali ikiendelea kuwa tete,
ambapo Jeshi la Polisi nchini limetangaza kumkamata mtu
anayetuhumiwa kueneza ujumbe wa uchochezi kwa kutumia simu ya mkononi.
Barabara nyingi za mjini Mtwara ziko tupu, huku
magari ya Jeshi la Wananchi na polisi yakiranda randa kuhakikisha
usalama, huku maduka na biashara nyingine zikiendelea kufungwa.
Wakati uhasama huo ukiendendelea, taarifa
zinaeleza kuwa vifo vimeongezeka na kufikia watu wat
atu, huku Mkuu wa Mkoa Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia, akisisitiza kuwa na taarifa rasmi ya kifo kimoja tu.
atu, huku Mkuu wa Mkoa Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia, akisisitiza kuwa na taarifa rasmi ya kifo kimoja tu.
“Mpaka sasa tuna taarifa ya kifo kimoja tu kupitia
utaratibu rasmi, kama kuna wengine wamekufa basi mtuletee taarifa kwa
kufuata utaratibu,” alisema Simbakalia.
Hata hivyo, taarifa za wananchi zilisema kuwa watu
wengine watatu walikufa kwa kupigwa risasi katika maeneo ya Mikindani,
huku baadhi ya wanawake wakidai kubakwa na polisi.
Wakati hayo yakiendelea, Jeshi la Polisi nchini
limetangaza kumshikilia mtu mmoja (jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za
kueneza ujumbe wa uchochezi na chuki kwa wananchi na viongozi wa
Serikali kwa kutumia simu ya mkononi.
Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa jana kwa vyombo
vya habari imeeleza kuwa meseji hizo zinaenezwa kwa lengo la kuchochea
fujo, vurugu na kutoa matusi kwa wananchi na viongozi wa Serikali.
Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema jana
kuwa mtu huyo amekuwa akifanikisha kazi hiyo kwa kutumia kadi 13 tofauti
za simu za mkononi.
“Alikamatwa akiwa na kadi 13 tofauti za simu za
mkononi, polisi bado inaendelea kumhoji mtu huyo na ushahidi
utakapokamilika atafikishwa mahakamani,” alisema Senso na kuongeza:
“Kwa muda mrefu sasa watu wa kada mbalimbali
nchini wamekuwa wakitumiwa ujumbe mfupi wa maneno katika simu zao,
unaohamasisha vurugu na uchochezi wa kidini, huku baadhi ya wananchi
wakizitupia lawama mamlaka husika kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.”
Jeshi hilo limewataka wananchi wenye taarifa
mbalimbali za wahalifu kama hao kujitokeza na kutoa taarifa hizo, ili
wanaotuhumiwa wasakwe na kukamatwa ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua
stahiki.
Wakizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya
Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, wananchi wengi wamelilalamikia Jeshi la
Polisi kwa kutumia nguvu kubwa katika utulizaji wa ghasia na kusababisha
vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.
0 comments:
Post a Comment