KAMPALA, Uganda.
NJEMBA mmoja amekutwa na rundo la kondomu tumboni mwake.Mtu huyo alikamatwa akiwa na dawa za kulevya aina ya nikotini tumboni mwake zikiwa ndani ya mipira ya kondomu.
Kwa sasa yupo chini ya ulinzi mkali wa polisi nchini Uganda, ambapo madaktari wanajaribu kuz
itoa tumboni.
Mtuhumiwa huyo ambaye ni raia wa Guinea, alitiwa mbaroni hivi karibuni. Tayari madaktari wameshamtoa kondomu takriban 21 zenye dawa kwa njia ya kutapika na haja kubwa.
“Mtu huyo alitapika kondomu 20 na baada ya kupewa dawa aina ya Bisacodyl alitoa kondomu nyingine moja kwa njia ya choo,” alisema daktari mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji.
Daktari huyo alisema anasikitika kuwa utaratibu wa kumtoa dawa hizo unachukuwa muda mrefu na kueleza kwamba acidi zinazomtoka mwilini zinaweza kudhoofisha mipira hiyo na kupasukia tumboni hivyo kuhatarisha maisha yake.
“Licha ya kumfanyia vipimo kadhaa, tumeshindwa kumfanyia upasuaji kwani hatujabaini ni wapi hasa mipira hiyo ilipo,” alisema daktari huyo.
0 comments:
Post a Comment