Watafiti waliochapisha matokeo ya utafiti wao katika jarida la PLOS ONE wanaobeba viini vinavyosababisha malari hhuwa na uwezo mkubwa wa kunusa .
Daktari James Logan kutoka chuo cha mafunzo ya afya mjini London anasema kuwa moja ya mabo ambayo humshangaza ni ambavyo viini vina kuwa na akil
i nyingi.
Alisema kuwa viini vinaonekana kuwa na akili nyingi kiasi cha kuwa mbele kwa fikira kuliko hata wanasayansi.
Katika kufanya utafiti wao wanasayansi waliwambukiza mbu na viini hatari vya Plasmodium Falciparum.
Wali wawekea mbu hao katika mkebe pamoja na soksi iliyo kuwa inavunda na ambavyo ilikuwa imevaliwa kwa masaa 20 mbu hao walijazana kwenye soksi hiyo wanasayansi walifanya utafiti huo na mbu walio kuwa hawana viini hivyo.
Waligundua kuwa mbu walio kuwa na viini waliweza kuvutiwa zaidi na soksi zilizo kuwa na uvundo.
Wanasayansi wana amini kuwa mbu walio kuwa na viini wanakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kunusa kwa sababu viini ndivyo vinawawezesha kunusa zaidi.
Kwa mbu binadamu anakuwa rahisi kushhambuliwa kwa sababu ya harufu ya mwiliwake na na kisha viinihhivyo vinavamia damu yake kuhakikisha kuwa vinaendelea kuuzaana .
Watafiti hao sasa watafanya utafiti wa miaka mitatu kuja kutaka ni vipi viini vina uwezo wa kufanya hivyo.
Daktari Logan anasema kuwa ikiwa wataweza kujua viini vinavyo sababisha malaria itawasaidia kupambana na ugonjwa wa malaria.
Kulingana na takwimu zaidi hivi karibuni shilika la afya duniani limesema kuwa mnamo mwaka 2012 takribani watu milioni 219 waliugua malaria huku wengine 660,000 wakilipotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo.
Afrika ndio bara lenye visa vingi vya watu kuugua malaria na asilimia tisini ya vifo vinavyo tokana na malaria hutokea barani humo .


0 comments:
Post a Comment