JESHI
la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia baadhi ya wanenguaji wa kundi
maarufu kwa kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kanga Moko na Laki si Pesa’, gazeti la
Tanzania Daima la leo lina hatimiliki ya hii habari.
Watuhumiwa
hao wamekamatwa sambamba na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao,
kufanya mapenzi hadharani na vitendo vya kishoga.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa kundi hilo sambam
ba na watu hao
walikamatwa katika maeneo ya Hoteli ya Travertine, Ambiance Club, Kinondoni
Makaburini, endelea kupitia na kukopi audifacejackson blog.Coco
Beach na Barabara ya Tunisia.
“Tumewakamata hao wanaofanya mchezo maarufu wa
Kangamoko na Laki si Pesa na tayari wanafikishwa mahakamani muda wowote na
msako bado unaendelea ili kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko
au baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia kutokana na mtindo wanaoutumia,”
alisema.
Kundi
la kangamoko limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara kutokana na kucheza
wakionesha maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi wanazozimwagia maji.
Kukamatwa
wasanii wa kundi hilo kumekuja siku chache tu tangu walalamikiwe katika Bunge
la Jamhuri ya Muungano kwamba wamekuwa wakipotosha jamnii.

0 comments:
Post a Comment