Maandamano ya May Day rally huko Jakarta, Indonesia, Mei mosi, 2013.
WAFANYAKAZI duniani kote wanaandamana mitaani Jumatano kuadhimisha siku ya kimataifa ya wafanyakazi duniani ijulikanayo kama Mayday huku wito ukitolewa kwa nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi.
Mgomo wa chama cha wafanyakazi Ugiriki siku ya may day umesababisha kadhia ya safari za feri kwenye kisiwa hicho na usafiri wa umma huko Athens ambapo waandamanaji wanaamdamana dhidi ya hatua zilizoongezwa muda za kubana matumizi kiuch
umi.
Wafanyakazi nchi nzima huko Spain ambako ukosefu wa ajira umeongezeka kufikia asilimia 27 wanafanya maanadamano kutaka mabadiliko ya sera za kiuchumi.
Huko Phillippines wafanyakazi wanaandamana huko Manila kudai serikali ilinde ajira zao. Pia wanaidai serikali kuacha kuajiri watumishi wa muda ambao hawapati haki sawa na wale wa kudumu.
0 comments:
Post a Comment