
mtoto akiwa
amebebwa na baba yake huku akipokelewa na nesi wa hospitali ya Mount Meru kwa
ajili ya kupelekwa kiwanja cha ndege cha Arusha kwa ajili ya kusafirishwa
kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Mmuhimbili jijini Dar es Salaam kwa
matibabu.
Na Mahmoud Ahmad Arusha
Wagonjwa saba ambao ni majeruhi wa mlipuko wa bomu kwenye kanisa la
Joseph Mfanyakazi eneo la Olasiti jijini Arusha wamehamishiwa kwenye Hospitali
za Muhimbili na LUgalo jijini Dar es Salaam.
Majeruhi hao wamesafirishwa mchana majira ya saa tisa kwa ndege ya
shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwenda kuendelea na matibabu zaidi baada
ya hali zao kuonekana bado zinahitaji vifaa vyenye uwezo wa hali ya juu.
Miongoni mwa walisafirishwa wapo watoto watatu wakike wawili na wakiume
mmoja huu wakina mama walisafirishwa wakiwa wawili na kinababa wawili ambao
hali zao bado mbaya licha ya matibabu walikuwa wakiyapata tokea juzi.
Wasamaria wema kutoka makampuni mbali mbali wameendelea kutoa misaada
mbali mbali ya hali na mali ikiwemo madawa na vifaa tiba na mablanketi na
mashuka,na Magodoro iliviisaidie hospitali za Mt.Meru na St,Elizabeth.
wakati huo huo wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
wamewatembelea wahanga wa bomu na kutembelea kanisa ambalo yalitokea maafa na
kujionea hali halisi wakiongozwa na spika wa bunge hilo Anna Makinda.
Miongoni mwa wabunge hao ni Mh.Habibu Mnyaa ambaye alisema kuwa hali
kama hiyo imewatia simanzi na kuiomba serekali kuchukuwa tahadhari kubwa kwa
matukio kama haya akiongea mbunge wa viti maalumu ccm vijana Catherine Maggige
alsema kuwa majeruhi hawa wanatia huruma na kuwa kitendo hicho kilichotokea
hakliwezi kuvumilika na kuiomba serekeli kuchukuwa hatua za haraka kukabiliana
na wimbi la tukio kama hilo.
Kwa upande wake spika makinda hakuweza kutoa
neno lolote bali aliingia kweny Gari teyari kwa safari ya kurudi Dodoma huku
akiwa na huzuni kubwa.

0 comments:
Post a Comment