Taarifa
za ndani kutoka kwa watu wa karibu na Mbunge huyo zinadai kwamba mbunge huyo
anajiandaa kuandaa utaratibu wa kupinga bajeti hiyo mpaka serikali itakapo leta
sheria mpya, “Serikali imegawa nakala za bajeti ya Nishati na Madini na wabunge
wote wanatakiwa kuhu
dhuria semina hiyo, lakini chakushangaza ni kwamba nakala
zote zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza"kilisema chanzo hicho.
Mbali
na mtoa taarifa hiyo kudokeza Habarimpya.com juu ya suala hilo Mbunge
huyo pia aliandika taarifa za kikao hicho katika ukurasa wake wa Facebook na
kudai kwamba hatua hiyo ya serikali inapaswa kupingwa kwa nguvu zote.
"Kati
ya Wabunge waliopinga hatua hiyo ni pamoja na Zitto Kabwe ambaye alisema kwamba
Gesi Asilia ipo kwenye rasimu na tayari imetangaza tena kugawa vitalu vya
mafuta na gesi kaskazini mwa Ziwa Tanganyika.endelea kupitia na kukopi
audifacejackson blog."Haraka hii ya serikali kugawa vitalu bila sera
wala Sheria inatoka wapi?
Nitashangaa sana wabunge kukimbilia posho za semina
hii na kuhalalisha maamuzi yasiyo zingatia maslahi ya Taifa kwa vizazi vya sasa
na vijavyo"alisema Zitto na kuongeza:
"Uamuzi
wa kugawa vitalu vipya bila kwanza kuwepo kwa sera na sheria mpya unapaswa
kupingwa kwa nguvu zote.kwani inabidi tuangalie ni wapi tunakwenda na kwa
manufaa gani baadae sio tu tuwe tunakimbilia posho".

0 comments:
Post a Comment