NI MATESO, DHULUMA NA UKATILI MTWARA...SOMA KISA HIKINAIBU Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF - Shaweji Mketo ametekwa na wanausalama na wanajeshi waliopiga kambi Mtwara MJINI.
Mketo alienda Mtwara MJINI jana
na Leo asubuhi alihudhuria mahakamani ambapo kesi ya Mwenyekiti wa
vijana CUF taifa (JUVICUF) Katani Ahmed Katani iliahirishwa.
Baada ya ahirisho hilo, Mketo alikutana na wanachama wa CUF walioko
Mtwara MJINI na kufanya nao kikao cha ndani. Katika kikao hicho
alielezwa namna wananchi wanavyoteswa kikatili na askari jeshi. Moja ya
jambo aliloelezwa ilikuwa ni juu ya mama mmoja aliyebakwa na askari na
kisha mamlaka zote zimekataa kumsaidia kuujulisha umma unyama
aliofanyiwa.
Mkurugenzi wetu Mketo alipojulishwa jambo hilo
aliomba akutane na mama huyo. Baada ya kikao, Mketo na viongozi
waandamizi wa wilaya akiwamo mhe. Kulaga ambaye ni katibu wetu wa wilaya
walianza safari ya kuelekea Msimbati ambako mama huyo amejisitiri baada
ya kubakwa na kunyimwa msaada na vyombo vilivyopaswa kumsaidia.
Mketo alifika Msimbati na kukutana na mama huyo na akachukua ushahidi
mbalimbali. Wakati wanarudi Mtwara MJINI ndipo walipotekwa na Askari
jeshi. Hivi sasa ukipiga simu za Mketo 0782 095 434 na ile ya Kulaga
0789 604968 zote zinapokelewa na askari jeshi na wanajibu kwa matusi ya
nguoni na kebehi za Hali ya juu.
Tumefanya juhudi za
kuwasiliana na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa polisi na serikali
bila mafanikio. Nimempata hewani RPC wa Mtwara ambaye anakiri kuwa
hajawashikilia viongozi wetu.
Nimemjulisha kama wako mikononi mwa
wanajeshi na wanausalama anasema hana mamlaka yoyote juu yao. HII ina
maana kuwa mkuu wa Jeshi la polisi wa mkoa Leo hana dhamana ya raia
wanaokamatwa na kuteswa katija eneo lake la kazi. Kama Leo Mtwara iko
chini ya Jeshi la wananchi na wanatesa watakavyo, Mbona rais hajatangaza
Hali ya hatari Mtwara??
Kwa taarifa zenye ushahidi, hadi sasa
askari jeshi hao wameshawakamata na kuwapeleka makambini zaidi ya
wananchi 100 ambapo wote hao wameteswa kinyama kwa kuvuliwa nguo zote,
kumwagiwa maji mwili mzima, kupakwa chumvi mwilini na kuanza kutandikwa
viboko vya miti maalum na kisha wakimaliza kuteswa huachiwa na
kurudishwa uraiani kuuguza vidonda vinavyotokana na vipigo.
Hakuna
utawala wa sheria Mtwara, ni ubabe, ukatili na dhuluma. Hakuna mahakama
wala JAJI, kila anayedhaniwa kuwa anapaswa kukamatwa lazima atakamatwa
na kamwe hapelekwi mahakamani, anateswa kikatili na kuachiwa.
Kwa namna askari waliowashikilia wanavyojibu kikatili, unaweza kupata
picha Mketo, Kulaga, dereva Kashinde na yeyote mwingine walivyo chini ya
mateso makali ya wanyama hawa.
Tunaposema kuwa nchi hii kuna
siku kila mtu atachoka tusilaumiwe. Siku hiyo itakapofika hatutasita
kuamuru raia wapambane na askari kila watakapowaona, tutakapofika hapo
nchi itabakia vipandevipande. Haiwezekani Leo kusini mwa Tanzania
kumegeuka sehemu ya mateso, ukatili na unyama.
Tunaendelea
kupambana kwa nguvu kuhakikisha kuwa serikali inawajibika, jeshi
linawajibika. Hatutakubali kuona uhuru na utu wa wananchi wa nchi hii
unapotezwa kwa faida za watu wachache.
Vyombo vya HABARI hivi
sasa haviripoti chochote kuhusu mateso ya wananchi Mtwara. Ripoti za
mateso ni Arusha, DSM na Mwanza. Nani atasimamisha ukatili huu wa watu
wasio na hatia kama siyo mimi na wewe ?.
Mawakili wetu pamoja na
mimi binafsi tunaelekea Mtwara kesho, lazima haki itendeke na
tutaitafuta haki kokote na kwa njia yoyote.
J. Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi CUF,
Tanzania Bara.
+255717536759.
CHANZO http://azimioletu.blogspot.com
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
1 comments:
hao wanaojiita wanasimamia haki za binadamu hawapo kazin?.kitindi
Post a Comment