SASA kuna kila dalili kuwa taifa la Afrika Kusini, limeanza kujiandaa
kukabiliana na tukio zito la kifo cha Rais wa Kwanza wa Taifa hilo,
Nelson Mandela (94), ambaye amelazwa kwa siku 18 hospitalini
akisumbuliwa na maradhi ya mapafu. Kauli tofauti kuhusiana na mwenendo
wa hali ya afya yake na matukio mbalimbali yasiyokuwa ya kawaida
yanayoripotiwa kufanywa na familia yake, ndiyo ambayo yameamsha hisia
hizo.
Taarifa zilizopatikana jana kutoka nchini Afrika Kusini, zinaeleza
kuwa watu muhimu katika familia ya Mandela, walikutana kwa dharura na
kufanya mazungumzo ya faragha katika kijiji alichozaliwa cha Qunu.
Wakati
wanafamilia hao wakikutana, msafara wa magari ya kundi jingine la
wanafamilia, ulitemb
elea eneo la makaburi ya ukoo wa Mandela.
Eneo hilo la makaburi ya ukoo lipo mita chache kutoka yalipo makazi
ya mdogo wake, Morris Mandela, mkabala na nyumba ya Mandela iliyoko
kijijini Qunu.
Haikufahamika mara moja mazungumzo ya wanafamilia
yalihusu jambo gani, lakini baadhi ya vyombo vya habari vya Afrika
Kusini, vililiripoti kuwa kwa mujibu wa mila na desturi za kabila la
Xhosa, wanafamilia hutembelea eneo la maziko iwapo kuna hisia za mmoja
wa wanafamilia kufariki dunia na wakati mwingine kufanya tambiko la
kimila.
Waliofika eneo la makaburi ni Winnie Madikizela-Mandela
ambaye ni mke wa zamani wa Mandela, Waziri wa Utumishi wa Umma, Lindiwe
Sisulu na Kiongozi wa chama cha upinzani cha United Democratic Movement,
Bantu Holomisa.
Msafara wao ulifika eneo la makaburi jana
asubuhi na kulikuwa na taarifa kuwa mtoto wa kike wa Mandela, Makaziwe
Mandela, aliitwa eneo hilo.
Waandishi wa habari walizuiliwa
kuvuka geti la eneo la makaburi hayo na waliofika nyumbani kwake Qubu,
walipigwa marufuku kusogea karibu na nyumba hiyo.
Wanafamilia
walioripotiwa kukutana kijijini Qunu ni Mandla Mandela, Thanduxolo
Mandela, Ndaba Mandela na Ndileka Mandela na Chifu Bhovulengwe wa Baraza
la AbaThembu.
Kikao hicho kinaeleza kuketi kuanzia saa nne
asubuhi, lakini baadhi ya wanafamilia waliotakiwa kukihudhuria
walichelewa kwa sababu ya kutopata taarifa mapema.
Familia yake yatoweka hospitali
Taarifa zinaeleza kuwa jana
hakuna ndugu wa Mandela aliyeonekana katika hospitali aliyolazwa,
isipokuwa timu ya madaktari wake ambayo iliwasili majira ya saa mbili
asubuhi.
Kutokuonekana kwa wanafamilia hao hospitalini hapo,
kulitafasiriwa kuwa ni kutokana na kikao kilichoitishwa Qunu. Napilisi
Mandela, ambaye ni kiongozi wa familia hiyo, alikaririwa na baadhi ya
vyombo vya habari akieleza kuwa familia ya Mandela inakutana kujadiliana
mambo mbalimbali yanayohusu afya ya mzee huyo.
Hata hivyo,
Napilisi Mandela, alieleza kikao hicho cha kifamilia kinahusu mambo ya
kimila na aliyekabidhiwa jukumu la kukiratibu ni Silumko Mandela.
Obama kutomuona
Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa Rais
wa Marekani, Barack Obama hatamtembelea Mzee Mandela hospitalini
alikolazwa mjini Pretoria, kwa sababu hakupangiwa kwenye ratiba yake.
Ratiba
ya Obama iliyotangazwa wakati wa ziara yake nchini Afrika ya Kusini,
inaonyesha kuwa atatembelea Kisiwa cha Robben ambako Mandela alifungwa
wakati wa harakati zake za kupigania uhuru.
Pia atatembelea mji maarufu wa weusi wa Soweto na Chuo Kikuu cha Cape Town, jijini Cape Town.
Daktari wake alonga
Timu ya madaktari wanaomtibu, jana ilitoa taarifa kuwa hali yake haijabadilika.
Rais Zuma awatuliza Waafrika Kusini
Rais Jacob Zuma
amelihutubia taifa kwa njia ya televisheni na kueleza kuwa hali ya Mzee
Mandela inaridhisha, huku akieleza pia kuwa maendeleo ya afya yake
hayafahamiki.
Zuma alisema hawezi kujua kama Mandela yuko kwenye
hali mbaya, kwa sababu yeye hajui mtu anayekuwa katika hali hiyo
anakuwaje, hivyo wenye nafasi ya kuzungumzia suala hilo ni madaktari
wake wanaomtibu.
Katika hotuba yake alisema hali ya Mandela
imekuwa ikibadilika badilika kila baada ya saa 24, hivyo ni jambo gumu
kujua kinachokuja mbele.
Zuma alimtembelea Mandela Jumapili akiwa ameambatana na Makamu wa Rais wa ANC, Cyril Ramaphosa.
CHANZO MTANZANIA.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment