ARUSHA.
WABUNGE wanne wa Chadema, Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu) wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na mkusanyiko usio halali kwenye Uwanja wa Soweto jana.

Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul
Chagonja alisema jana kwamba pamoja na wabunge hao pia wamewakamata watu
wapatao 60 kutokana na vurugu zilizoz
uka jana baada ya Polisi kuwatawanya kwenye uwanja huo waliokuwa wamekusanyika kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea kwenye uwanja huohuo, Jumamosi iliyopita.

Mbali ya viongozi hao, alisema wanawasaka Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
“Tunawasaka wabunge ili tuwajumuishe na watu hawa
kwa kosa la kuhusika na mkusanyiko usiokuwa halali. Hadi sasa
tumefanikiwa kulinasa gari la Mbowe,” alisema Chagonja.
Pia kamatakamata hiyo imemkumba Mpigapicha wa
Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Ashraf Bakari. Polisi
walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya waombolezaji hao.
Awali, Kamishna Chagonja alisema jana asubuhi kuwa
wamelazimika kuzuia viwanja hivyo kutumika baada ya wamiliki wake, AICC
kuzuia shughuli za Chadema kwenye eneo lao.
Kamishna Chagonja aliwaonyesha waandishi wa habari
barua aliyosema imeandikwa na uongozi wa AICC kuzua Chadema kuendelea
kuutumia Uwanja wa Soweto.
Mabomu yarindima
Dalili za kuzuka kwa vurugu zilianza kuonekana
asubuhi baada ya polisi kuzingira uwanja huo na kuzuia watu waliokuwa
wameanza kufurika katika eneo hilo kuanzia saa moja kuingia kwa ajili ya
maombolezo.
Wakati Polisi wakiwa uwanjani, wananchi walijaa nje ya uwanja na kuonekana kama wamewazingira.
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe
waliwasili uwanja hapo yapata saa nane mchana na kukuta zuio hilo na
kuanza kuzungumza na wananchi ingawa FFU walikuwa wakiwataka watu
kutawanyika.
Mabomu yalianza kurindima wakati Arfi aliposimama na kuwahimiza wananchi kuelekea Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuaga miili ya marehemu.
Mabomu yalianza kurindima wakati Arfi aliposimama na kuwahimiza wananchi kuelekea Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuaga miili ya marehemu.
“Tuna muda mfupi sana wa kuzungumza hapa, tunaomba
wote tuelekee Hospitali ya Mount Meru kuaga miili ya marehemu kwa
sababu uwanja huu umezuiwa na polisi,” alisema Arfi kabla ya kukatishwa
na milipuko ya mabomu.
CHANZO MWANANCHI.
CHANZO MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment