BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

GESI YAMFIKISHA KORTIBU MBUNGE WA CCM MTWARA.

Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini,Hasnein Murji akiongoza msafara wa wazee wa Mtwara na Masheikh wa mkoa huo walipokuwa wakiingia nyumbani kwa Mbunge wa jimbo la Mtama,Bernard Membe kwa ajili ya hafla fupi yakuukaribisha 2012, Mbunge huyo uchochezi na kusababisha vurugu za kupinga mradi wa bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam.


MBUNGE wa Mtwara Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasnain Murji, amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara kujibu mashitaka ya uchochezi na kusababisha vurugu za kupinga mradi wa bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidi Mwandamizi, Dainess Lyimo, kisha akasomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Kisheni Mutalemwa.

Wakili Mutalemwa alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 19, mwaka huu katika eneo la Ligula Mjini Mtwara chini ya kifungu 390 cha adhabu.

Mshtakiwa huyo alikana mashitaka na kupelekwa rumande baada kushindwa kutimiza moja ya mash

arti ya dhamana ya kuwasilisha hati ya kusafiria mahakamani hapo yaliyotolewa na Hakimu Mutalema.
Masharti mengine aliyopewa ni  kupeleka mdhamini mmoja, Mkazi wa Mji wa Mtwara mwenye mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh. milioni 20.

Awali, Hakimu Mutalemwa alisema endapo mshtakiwa huyo atapatiwa dhamana, hataruhusiwa kuendesha mikutano ya hadhara bila kupata kibali kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara.

Awali wakili wa utetezi, Henry Chaula aliiomba mahakama hiyo kumuachia huru mteja wake kwa dhamana ingawa hakuwa na hati ya kusafiria mahakamani hapo.

Wakili Chaula alidai kuwa kutokana na hadhi ya mshtakiwa huyo kuwa mwaminifu na kiongozi wa kuchaguliwa na wananchi, ikiwa ni pamoja na kujisalimisha mwenyewe kituo cha polisi baada ya kutafutwa na jeshi hilo, anaiomba mahakama hiyo kumwachia  kwa dhamana na kutoa kibali cha kuwasilisha hati hiyo ya kusafiria siku inayofuata (leo).

Ombi hilo liligonga mwamba kutokana na mahakama kuendelea kumnyima dhamana mshtakiwa huyo kwa kushindwa kutimiza sharti la kuwasilisha pasi yake ya kusafiria na kurudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa kesho.

Mshtakiwa huyo alipelekwa mahabusu katika gereza la Lulungu kwa gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser chini ya ulinzi mkali wa askari wa jeshi hilo.

Murji na washtakiwa wengine 91 walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka hayo. Baadhi yao waliachiwa kwa dhamana na wengine kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti hayo.

Wengine waliofikishwa mahakamani hapo hivi karibuni ni viongozi wa vyama vya upinzani.

Washtakiwa hao ni  Katani Ahmed Katani, Said Kulaga wa Chama Cha Wananchi (CUF), wengine ni Hassan Uledi wa NCCR- Mageuzi na Hamza Licheta wa Tanzania Labour Party (TLP), wote ni wakazi wa Mtwara.

Washtakiwa hao wanadaiwa kula njama, kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivi walikana mashtaka hayo.

Tangu kutokea kwa vurugu hizo mkoani humo Novemba 16, mwaka jana hadi sasa zimesababisha baadhi ya watu kupoteza maisha huku wengine wakiachwa majeruhi na mali nyingi kuharibiwa.

Mvutano uliopo sasa kati ya Serikali na Wananchi wa Mtwara ni usafirishwaji wa  gesi kutoka mkoani humo kwenda Jijini Dar es Salaam kwa njia ya bomba, huku serikali ikitaka gesi hiyo ipelekwa Dar es Salaam wakati wananchi wa Mtwara wakitaka ibaki mkoani humo.

HALI YA MAHAKAMA.
Jana majira ya saa 2 asubuhi magari ya polisi yalitanda mahakamani hao huku yakiwa na askari ambao waliimarisha ulinzi na kutawanya wananchi waliojitokeza kufuatilia kesi hiyo.

Baadhi ya askari walikuwa na mbwa na wale wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakizunguka kwenye viwanja vya mahakama hiyo.

Wananchi ambao walifurika mahakama hapo tangu asubuhi kwa lengo la kusikiliza kesi hiyo, hawaruhusiwa kwa kile kilichoelezwa na polisi kuwa hawakutakiwa kuwapo kundi la watu katika maeneo hayo.

“Hatuhitaji mkusanyiko wa watu hapa mahakamani, tuwaombeni sana wananchi wote ruduni majumbani mwenu anayeruhusiwa kuingia huku ndani ni mtu ambaye amekuja na barua kutoka kwa mtendaji wa kata kwa ajili ya kutoa dhamana,” alisema mmoja wa askari hao.

Wananchi hao watii amri hiyo na kutoka katika eneo la mahakama hiyo huku baadhi yao wakilalamika kunyimwa uhuru wa kusikiliza kesi za ndugu zao.

HALI YA SOKO
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko kuu la mjini Mtwara, walifunga biashara zao kwa kuhofia kukamatwa na polisi endapo vurugu zingetokea.

Wafanyabiashara wa nyanya na matunda, walionekana wakiendelea na biashara zao, huku maduka yakiwa yamefungwa.
 
USAFIRI
Kwa upande wa usafiri wa mabasi ya kwenda wilayani na baadhi ya mikoa jirani, ulisitishwa huku wananchi wakihangaika kusaka huduma hiyo bila ya mafanikio.

Mabasi yanatoa huduma za usafiri kati ya Dar es Salaam yaliondoka mapema yakiwa na abiria.  

CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: