BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KESI YA UAMSHO YASTAJABISHA.

Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI),  Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake wakiwa katika gari la Polisi. Picha Maelezo Zanzibar.

ULINZI umeimarishwa Mahakama ya Rufani nchini, wakati wa usikilizwaji wa ombi lililowasilishwa na viongozi wa Jumuia ya Uhamsho na Miadhara iliyokatwa na kiongozi wa jumuia hiyo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake tisa dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar.

Sanjari na hilo, washtakiwa hao hawakuwepo mahakamani hapo, bali mawakili wao tu ndiyo walikuwepo, kitu kilichowafanya baadhi ya watu waliyokuja kusikiliza rufaa hiyo kupigwa butwaa.

Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa na mabomu ya machozi walizunguka eneo la mahakama hiyo kwa kuimarisha usalama, ambapo watu waliyokuwa wakii
ngia katika geti la mahakama hiyo walikuwa wakikaguliwa kwanza ndiyo waingie.

Pia baadhi ya waandishi wa habari walitakiwa kutoa vitambulisho kwa wakaguzi hao ili waweze kujiridhisha kama kweli ni waandishi wa habari kama walivyodai.

Upande wa waoombaji (Uhamsho) waliwasilisha ombi lao mbele ya  jopo la majaji watatu, ambao ni January Msoffe, Salum Massati na William Mandia kupitia mawakili wao.

Mbali ya Sheikh Ahmed, waombaji wengine ni Mselem Ali Mselem,  Mussa Juma Mussa, Azan Khalid, Suleiman Juma Suleiman, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman, Ghalib Ahmada Juma, Abdallah Said na Fikirini Fikirini.

Sheikh Ahmed na wenzake wanaiomba mahakama hiyo, itoe amri ya kuifuta rufaa iliyowasilishwa na DPP, Aprili 15, ya mwaka huu, kwa sababu hadi sasa hakuna rufaa iliyokuwa imefunguliwa mahakamani ya kupinga amri ambazo zilitolewa na mahakama.

Watuhumiwa hao waliwasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura na wameonesha tangu, Oktoba 25 mwaka 2012  hadi sasa wanaishi gerezani na maombi hayo yatachelewesha kusikilizwa hivyo yakicheleweshwa kusikilizwa yatasababisha waendelee kusota gerezani kwa muda mrefu hivyo kuwaletea madhara na usumbufu.

Sheikh Ahmed anadai taarifa ya kukata rufaa ya DPP haihusiani na uamuzi ulitolewa Machi 11, mwaka huu, ambao mdaiwa (DPP), anaupinga.

Anadai katika maombi ya DPP hayajaambatanishwa na kiapo cha mwapaji, ambapo mwapaji ni wakili wa Sheikh Ahmed, Abdallah Juma Mohammed, ambaye anadai Oktoba 25, mwaka 2012, waombaji walishitakiwa kwa makosa manne chini ya sheria ya Usalama wa Taifa na Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

Wanadai kuwa, mashtaka dhidi yao walisomewa mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar siku hiyo, lakini hawakupewa nafasi ya kujibu kwasababu msajili hana mamlaka ya kusikiliza mashitaka hayo.   

Wakili Abdallah anadai waombaji waliomba kudhaminiwa mbele ya msajili, ambapo Wakili wa Serikali alipinga maombi hayo kwa msingi wa kuwa kuna hati ya DPP wa Zanzibar chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa kwamba usalama wa nchi ungetetereka hivyo mahakama isiwape dhamana.   

Alidai Msajili aliwanyima dhamana wateja wake na kuwaamuru warudi rumande hadi Novemba 8, mwaka 2012, kesi ilipokuja kwaajili ya utajwa.   

Kwa mujibu wa wakili huyo, waombaji hawakuridhika na uamuzi na kuwasilisha maombi ya marejeo ya uamuzi Mahakama Kuu ya Zanzibar, lakini mlalamikiwa aliwasilisha pingamizi la awali akiomba mahakama itupilie mbali maombi hayo.

Anadai baada ya Jaji Abraham Mwampashi wa Mahakama Kuu  kusikiliza maombi ya marejeo na pingamizi la awali la DPP, Machi 11, mwaka huu, alitoa uamuzui wa kutupilia mbali pingamizi na kufuta mwenendo mzima uliokuwa chini ya msajili na uamuzi wa maombi ya dhamana.

Wakili huyo anadai Machi 12, mwaka huu, DPP aliwasilisha taarifa ya kukata rufani kupinga uamuzi wa Jaji Mwampashi kutupilia mbali pingamizi lake la awali na kuwasilisha sababu za kukata rufani.

Hata hivyo, wakili huyo anadai uamuzi wa Mahakama Kuu wa Machi 11, mwaka 2013, hauwezi kupingwa kwa njia ya rufani wala ya marejeo mbele ya Mahakama ya Rufani.
chanzo JAMBOLEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: