BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MABAO 31 YATINGA KATIKA NYAVU HATUA YA NANE BORA MTOANO MASHINDANO YA TIKA CUP 2013 MOROGORO.

Mshambuliaji wa timu ya soka ya kata ya Kihonda, Ulimboka Mwakingwe mbele akimtoka mlinzi wa Mazimbu wakati wa mashindano ya TIKA CUP 2013 katika uwanja wa Kilakala Makaburini ambapo katika mchezo huo Kihonda iliibuka na ushindi wa bao 6-1 katika hatua ya 16 bora mtoani mkoani Morogoro. JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM

Na Juma Mtanda, Morogoro.
JUMLA ya mabao 31 yamezamishwa nyavuni huku bao 27 yakichikwa kwa njia ya mikwaju ya penalti tangu kuanza kwa mashindano ya TIKA CUP 2013 Manispaa ya Morogoro katika hatua mbili za awali na 16 bora ambapo michezo hiyo ilianza kutimua vumbi juni 6 mwaka huu kwa kushir
ikisha timu 24 za kata inayounda Manispaa hiyo katika viwanja viwili tofauti vya Shujaa na Kilakala makaburini mkoani hapa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa, Mwenyekiti wa mashindano ya TIKA CUP 2013 Manispaa ya Morogoro, Msifuni Chenjela alisema kuwa mpaka sasa tayari michezo 18 imechezwa kwa michezo ya hatua ya awali na hatua ya 16 bora huku washambuliaji, Wida Jumanne wa timu ya Gereji akiongoza kwa kupachika bao matatu kati ya mabao 31 yaliyofungwa katika michezo hiyo.

Chenjela alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuhamasisha wananchi kujiunga katika mfumu wa tiba kwa njia ya kadi kutoka mfuko wa afya ya jamii inayomtaka mwananchi kuchangia sh10,000 ili kupata huduma hiyo kwa mwaka katika vituo vya afya na zahanati ndani ya Manispaa ya Morogoro na malengo mengine yamelenga kuendeleza vipaji vya mchezo huo kwa vijana wanaoshiriki mashindano hayo na mashabiki kupata burudani baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara.

Kati ya michezo yote 18 ni mabao 31 ndiyo washambuliaji wamefunga huku bao 27 yakifungwa kwa mikwaju ya penalti baada ya kutokea madhambi katika maeneo ya hatari na waamuzi kutoa adhabu hizo na kuzaa mabao hayo na  tathimini ya awali inaonyesha walinzi wamekuwa wakifanya makosa mengi maeneo ya hatari huku washambuliaji wakionekana kuwa butu baada ya kufunga mabao sita.

Mashindano yamekuwa na msisimuko wa hali ya juu sana kutokana na matukio mbalimbali ndani na nje ya uwanja lakini tumefanya tathimini ya michezo ya hatua hizi mbili tumebaini kuwa makocha wana kazi ya ziada ya kuwanoa washambuliaji wao ili waweze kupachika bao, kuna michezo 18 lakini washambuliaji wa timu hizo wamefunga bao sita huku 27 zikifungwa kwa penalti hawa washambuliaji wanakosa mbinu ya kufunga ?. alihoji Chenjela.

Timu zilizofuzu kutinga hatua ya nane bora mtoani ni pamoja na Terminal itayochuana na Mwembesongo katika uwanja wa Shujaa huku Boma ikionyeshana kazi na Kingo uwanja wa Kilakala Makaburini ambapo michezo yote itaanza majira ya saa 10 jioni leo (jana) ili kupata timu nne ambazo zitachuana katika mfumo wa ligi ili kupata mshindi wa kwanza, pili na tatu wakati leo Gereji itacheza na Kihonda uwanja wa Shujaa na Mzinga ikicheza na Sabasaba uwanja wa Kilakala Makaburini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: