KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa kijana umezikwa mara
mbili, baada ya maziko ya kwanza kufanywa na wanakijiji cha Mwalubungwe
Kata ya Hungumalwa Kwimba, Mwanza, baada ya kumuua wakidhani jambazi na
kumzika bila nguo wala sanda.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, baba mzazi wa kijana huyo, Seni
Kamera alisema mwanawe Valence Abel (23), mkazi wa Zunzuli, Shinyanga,
alikuwa akiishi Kahama kwa mganga wa kienyeji, akipata matibabu ya
upungufu wa nguvu za kiume.
Alisema mwanawe huyo aliishi kwa mgan
ga huyo kwa miaka miwili bila
kurudi nyumbani.
Alidai wiki mbili zilizopita, aliamua kuondoka kwa
mganga huyo kwa miguu akiwa amefuga ‘rasta’ na kuvaa kaniki na ngozi,
masharti ambayo alipewa na mganga wake ili tatizo lake liweze
kumalizika.
Alisema akiwa njiani kurudi nyumbani, alifika katika kijiji cha
Mwalubungwe, na kwenda nyumba ya mkazi wa kijiji hicho kuomba chakula
kutokana na njaa.
“Alipofika katika nyumba hiyo alikuta watoto wanacheza nje.Kwa
mwonekano aliokuwa nao, walimpiga kwa mawe na kumwita mwizi, kisha mzazi
mmoja akapigana naye huku akipiga kelele, watu walifika na kumshambulia
na hatimaye alipoteza maisha na kumzika bila nguo wala sanda,“ alisema
Kamera.
Alisema taarifa za kifo cha mwanawe, alizipata kwa mtu aliyemwambia kuna mtu ameuawa ambaye alijitambulisha kwa jina la Kamera.
Alifuatilia na kufukua kaburi hilo na kukuta ni mwanawe. Alichukua maiti na kumzika tena.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alipohojiwa kuhusu
tukio hilo, alisema hana taarifa. Lakini, aliahidi kufuatilia ili
kufahamu undani wake.
CHANZO HABARILEO.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment