BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAJANGA: MCHUNGAJI ADAIWA KUTEMBEA NA WAUMINI WAKE AMBAO WAMEOLEWA NA KUWAPA MIMBA.

MCHUNGAJI mmoja wa kanisa la Church elders of Faith Ministries Nchini Zimbabwe amejikuta akivuliwa wadhifa wake huo mtakatifu mara baada ya kugundulika kuwapa mimba wake za watu sita katika nyakati tofauti tofauti ndani ya mwaka mmoja. 

"Kitu alichokifanya mchunagaji huyu ni kibaya sana na mtu kama yeye hatakiwi kabisa kuwa sehemu ya kanisa kwa sasa, kwasababu kile alichokifanya ni kinyume kabisa na maadili ya UKRISTO.

Kuna baadhi ya watu wenye hasira kali walitaka kumpiga lakini bahati nzuri wazee wa kanisa waliwazuia "..alisema mmoja wa waumini wa kanisa hilo aliyeonekana kuchukizwa na kitendo cha mchungaji huyo.

Wahubiri katika kanisa hilo walivujisha kuwa katika kanisa hilo kuna kiongozi mkubwa ambaye ana tabia ya kulala na wake za watu na alipokuja kuulizwa kuhusiana na hilo mchungaji huyo alikuwa na haya ya kusema.
 
"Najisikia vibaya sana na ningependa kuomba msamaha kwa hili nililolifanya na kama nikipewa nafasi nyingine naahidi kutorudia tena. 
 
Vile vile nakubaliana na maamuzi ya wazee wa kanisa kuamua kunivua wadhifa wangu mtukufu"... alimalizia mchungaji huyo ambaye alionekana kuwa na majonzi ya kutosha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: