MAMA wa marehemu Langa Kileo,
Vanessa Kimei (pichani) amefungua kinywa chake na kusema kifo ni mipango ya
Mungu lakini kama angekuwepo nyumbani kwake Mikocheni, Dar, mwanaye asingekufa
haraka kiasi hicho.
Akizungumza na Amani hivi karibuni,
Mama Langa alisema wakati mwanaye alipoanza kuugua hadi kupatwa na umauti Juni
13, mwaka huu, yeye alikuwa safarini nchini Marekani kum
uona mwanaye mwingine
aliyekuwa amejifungua.
“Wakati mwanangu ameanza kuumwa
sikuwepo, nilikuwa safarini Marekani nilikoenda kumuona mwanangu wa kike
aliyekuwa amejifungua, kwa mila za kwetu ni lazima mama kwenda kumuogesha mtoto
lakini ningekuwepo mwanangu asingeondoka jamani,’’ alisema mama Langa.
Akifafanua
kauli yake, mama huyo alibainisha kuwa kipindi alipokuwa akiishi na mwanaye
kabla hajasafiri, mara nyingi alikuwa akimhudumia alipokuwa akiumwa hivyo hata
katika ugonjwa uliosababisha mauti yake basi angeweza kumtibu yeye mwenyewe.
Alisema
kuwa wakati mwingine alikuwa akimuwekea hadi dripu za dawa akiwa pale nyumbani
na kunusuru maisha ya mwanaye lakini ghafla kifo kimetokea wakati yeye hayupo.
“Nilikuwa
namuwekea dripu za dawa mwanangu hapahapa nyumbani, alikuwa anaugua kwa muda na
kisha anarudi katika hali ya kawaida,” alisema kwa uchungu mama Langa.
Hata
hivyo baadhi ya waombolezaji waliokuwepo msibani walimsihi mama huyo
kukubaliana na mipango ya Mungu kwamba kila mwanadamu lazima atakufa, hali
iliyompa faraja na kumfanya anyamaze.
Marehemu
Langa aliyefariki baada ya kusumbuliwa na kile kilichoelezwa kuwa ni ugonjwa wa
malaria kali na homa ya uti wa mgongo, alizikwa Jumatatu iliyopita katika
Makaburi ya Kinondoni, Dar.
Na Mwaija Salum wa GPL.

0 comments:
Post a Comment