Mtoto akiweka kadi kumtakia Mandela apone haraka nje ya hospitali ya Mediclinic Heart, ambapo Mandela amelazwa.
Binti wa Nelson Mandela anasema kiongozi huyo wa zamani wa Afrika kusini yupo katika hali mahututi.
Makaziwe Mandela alizungumza kwenye radio ya taifa Alhamis wakati
wanafamilia walipokusanyika kwenye hospitali ya Pretoria Mediclinic
Heart ambapo Bwana Mandela amelaz
wa kwa siku ya 19 sasa.
Rais Jacob Zuma aliahirisha safari yake kuelekea Msumbiji Jumatano baada ya kumtembelea Mandela hospitali.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Barack Obama yupo nchini Senegal kwenye
kituo chake cha kwanza katika ziara yake barani Afrika ya kuhamasisha
biashara, uwekezaji na usalama wa chakula.
Ajenda zake alhamis zinajumuisha mikutano na dhifa rasmi ya chakula cha
jioni na Rais wa Senegal Macky Sall pamoja na mazungumzo ya utawala wa
sheria na viongozi wa mahakama katika eneo.
Bwana Obama na mke wake Michelle pia watatembelea kisiwa cha Goree, eneo
la UNESCO World Heritage ambalo kutoka karne ya 15 hadi 19 lilikuwa
kituo kikubwa cha biashara ya utumwa kwenye pwani ya Afrika.
Kutoka nchini Senegal, bwana Obama anapanga kuelekea Afrika kusini na
kutembelea kisiwa cha Robben, gereza ambalo rais wa zamani wa Afrika
kusini Nelson Mandela alifungwa kwa takribani miongo miwili.
Pia
atasimama nchini Tanzania kabla ya kurejea nyumbani nchini Marekani.
CHANZO http://www.voaswahili.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment