BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MANISPAA, MOROGORO VIJIJINI WANYANYASA KWA KUTWAA MAKOMBE UMISSETA 2013.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Said Amanzi akimkabidhi kombe nahodha, Jimmy Michael wa Manispaa ya Morogoro baada ya kuifunga Mvomero katika mchezo wa soka wa fainali mashindano ya Umisseta ngazi ya mkoa yaliyo
fikiwa tamati kwa michezo mbalimbali uwanja wa jamhuri Morogoro kwa kuibuka na ushindi wa penalti 7-6. 

Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU ya soka ya wavulana ya Manispaa ya Morogoro imetwaa ubingwa wa mashindano ya michezo ya shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya mkoa baada ya kuibuka kidedea dhidi ya mahasimu wao Mvomero katika mchezo wa fainali kwa penalti ya bao 7-6 katika hitimisho la michezo hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa. 

Manispaa ambayo imeivua ubingwa mabingwa watetezi vijana wa mkuu wa wilaya Kilombero, Hassan Mallasa Kilombero kwa kuitandika bao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali ilianza mchezo huo wa fainali kwa kasi na kulishambulia lango la wapinzani wao katika vipindi vyote lakini safu ya ushambuliaji wa timu hiyo ilishindwa kupenya ngome ya vijana wa mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka na mchezo huo kumalizika kwa sare tasa ya 0-0 na bingwa kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti. 

Mshambuliaji, Benard Joseph ndiye aliyekuwa shujaa kwa Manispaa kwa kuipatia ubingwa wa Umisseta 2013 timu yake katika penalti nane zilizopigwa huku Manispaa wakipoteza moja kupitia mchezaji, Stawa Francis wakati Mvomero wakipoteza penalti mbili za wachezaji, Ramadhan Yusuph na William Chidundo ambapo idadi ya kupigwa panalti nane ilikuja baada ya kwenda sare ya bao 4-4 katika penati tano za kwanza na kufikia hatua ya kupigwa mchezaji mmoja mmoja. 

Morogoro Vijijini ndiyo waliofanikiwa kutwaa ubingwa soka kwa upande wa wasichana baada ya kuilaza Kilosa nayo kwa changamoto ya mikwaju ya penalti ya bao 3-1 huku Kilosa wakipoteza mikwaju minne na mabingwa wakipoteza mikwaju miwili kufuatia kwenda sare tasa ya 0-0 na kuamuliwa ubingwa kuamuliwa kwa njia hiyo. 

Wakati Manispaa ikitwaa ubingwa upande wa soka wavulana, Morogoro Vijijini ilitwaa ubingwa wa soka kwa upande wa wasichana huku katika mchezo wa basketiboli, Manispaa ilitwaa ubingwa huo baada ya kukusanya pointi tisa ikifuatiwa na Kilombero yenye pointi sita wakati upande wa wasichana Morogoro Vijijini nayo ilitangazwa mabingwa na katika mchezo wa neriboli Morogoro Vijijini nayo iliendelea kuibuka na ubingwa wa mchezo huo. 

Kwenye mchezo wa wavu wavulana timu ya Manispaa iliendelea kutamba kwa kuibuka na ubingwa wa mchezo huo wakati kwa wasichana Kilombero ndiyo mabingwa huku Ulanga ikiibuka kidedea kwa kutwaa ubingwa wa jumla katika mchezo wa riadha.


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: