Na Juma Mtanda,
Morogoro.
MASHINDANO ya TIKA
CUP 2013 yameanza kutimua vumbi juni 6 kwa kushirikisha timu 24 za kata
zinaunda Manispaa ya Morogoro katika viwanja wa Shujaa na Kilakala makaburini
mkoani hapa.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hii mjini hapa Mwenyekiti wa mashindano hayo, Msifuni
Chenjela alisema kuwa mashindano hayo yameanza kutimua vumbi juni 6 na
yanatarajia kumalizika juni 30 mwaka huu ikishirikisha timu zinazounda Manispaa
ya Morogoro.
Chenjela alisema
kuwa mashindano hayo yanaendeshwa kwa mfumo wa mtonani ambapo kumegawanywa
katika makundi mawili, A na B na michezo ya kundi A inafanyika uwanja wa Shujaa
wakati kundi B wanatumia uwanja wa Kilakala Makaburini ambapo kila kundi itatoa
timu nne ambao nazo zitachuana kwa mfumo huo huo wa mtoano.
“Haya mashindano
yana lengo la kuhamasisha wananchi kujiunga katika mfumu wa tiba kwa njia ya
kadi kutoka mfuko wa afya ya jamii inayoka mwananchi kuchangia sh10,000 ili
kupata huduma hiyo kwa mwaka katika vituo vya afya na zahanati ndani ya
Manispaa ya Morogoro” alisema Chenjela.
Chenjela alisema
kuwa mashindano hayo kwa sasa tayari yamefikia hatua ya nne bora kwa kila kituo
ambapo timu hizo zitashindanishwa kwa
michezo ya nane bora na timu nne ambazo zitafuzu zitacheza katika mfumo wa ligi na kupata washindi akiwemo
wa kwanza, pili na tatu.
Chenjela alisema
kuwa bingwa wa mashindano hayo atakatiakana juni 30 na julai mosi ndiyo zawadi
za washindi zitatolewa katika wa kilele za maadhimisho ya siku ya serikali za
mitaa ambazo zitafanyika kitaifa mkoani Morogoro.
Alitaja zawadi
washindi wa mashindano hayo kuwa ni sh500,000 na ngao kwa mshindi wa kwanza, sh
250,000 mshindi wa pili na mshindi wa tatu ataambulia sh 150,000.

0 comments:
Post a Comment