Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akikagua Gwaride la Mapokezi mara
alipowasili katika Makao makuu ya Jeshi la Oman kuanza Ziara ya kikazi
nchini Oman, kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Oman Luteni Jeneral Ahmed bin
Harith Al Nabhani.
Mkuu wa Majeshi akiwa katika mazungumzo na Mwenyeji wake.
Mku
wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange katikati) akiwa katika mazungumzo
na Waziri katika Ofisi ya Mfalme Mhe. Sultan bin Mohamed Al Nuam
ani (kulia), akishuhudia ni Balozi wa Tanzania nchini Oman Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh (kushoto)
ani (kulia), akishuhudia ni Balozi wa Tanzania nchini Oman Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh (kushoto)
Mkuu
wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akipokea taarifa kutoka kwa
Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Balozi Ali Ahmed Saleh
alipotemb
elea ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Oman.
elea ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Oman.
Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh akimuonyesha Mkuu wa Majeshi mchoro wa litakalokuwa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Oman.
Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh mstari wa mbele kulia akiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa majeshi na ujumbe wake.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo cha Uongozi na kamandi cha Oman.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana na Meja Saif Wibonela, Mwanafunzi wa kitanzania anaesoma hapo.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange (watano kutoka kushoto waliokaa ) katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo cha Anga cha Oman (watatu kutoka kushoto waliokaa) ni Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Balozi Ali Ahmed Saleh.
Mkuu
wa majeshi ya Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, alifanya ziara ya
Kikazi nchini Oman kuanzia tarehe 23 hadi 27 Juni 2013 kwa Mwaliko wa
mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani.
Ziara
hii ilikuwa na madhumuni makuu ya kuimarisha uhusiano wa kindungu
uliopo baina ya Oman na Tanzania kupitia sekta ya ulinzi na kuanzisha
uhusiano wa karibu na ushirikiano baina ya vyombo hivi vya ulinzi kati
ya Tanzania na Oman.
Katika
ziara hii Mhe. Jenerali Mwamunyange alikutana na kufanya mazungumzo na
Mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani na pia
kukutana na Waziri katika Ofisi ya Mfalme Mheshimiwa Luteni Jenerali
Sultan bin Mohamed Al Nuamani .
Mbali
na kukutana na viongozi hawa wa Oman, Mkuu wa majeshi alipata nafasi
kutembelea maeneo kadhaa kujonea shughuli mbalimbali za Jeshi la Oman,
alitembelea makumbusho ya Jeshi la Oman, Chuo cha Uongozi na kamandi cha
Oman, Chuo cha Jeshi la Anga, Hospital ya Jeshi , Makao makuu ya Jeshi
la Askari wa Miguu pamoja Makao makuu ya Jeshi la Majini.
Katika maeneo yote aliyotembelea Mheshimiwa Mkuu wa Majeshi alifurahishwa sana na shughuli za jeshi la Oman na kuridhika na hatua iliyopigwa na Jeshi la Oman. Mkuu wa majeshi pia alitembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman kujionea shughuli mbalimbali za Ubalozi na pia kuhudhuria hafla ya chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa heshima yake nyumbani kwa Mheshimiwa Balozi.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment