BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MSANII WA KIZAZI KIPYA ATANGAZA KUACHA KUBWIA UNGA NCHINI KENYA.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Kenya Ibra Da Hustler akiwa katika pozi 

WAKATI kesho dunia inaadhimisha siku ya matuizi ya dawa za kulevya Rapper Ibra Da Hustler amefunguka kuwa sasa anampango wa kubadilisha maisha yake kwa uamuzi aliouchukuwa wa kuachana na matumizi ya dawa aina ya Herion na Crack Cocaine.

Da Hustler ameamua kuachana na matumizi hayo ya dawa za kulevya baada ya kuona kuwa ni uharibifu wa pesa pili kitendo hicho ni kukaribisha dharau kwenye maisha yake huku akihatarisha maisha, Rapper huyo ambaye kwa sasa ana takribani siku nne hajagusa toka amejiunga na taasisi amejif
unza kuvumilia na matumaini yake ni kuachana kabisa na matumizi hayo ya dawa za kulevya.

Akizungumza na habarimpya.com alisema kwamba mwanamke ndiye aliyemshawishi mpaka akiingiza katika matumizi ya dawa ya kulevya. “Kuna binti alinishawis kutumia dawa na ndio nikajikuta nimeingia katika mkumbo huu najuta kumfahamu nakubaini kuwa hataki maendeleo yangu kabisa nanimejifunza kutoka kwake, sasa nikimwambia mtu usiguse dawa ataamini kwani najua kitu gani atapata kwenye maisha yake”alisema Dar Hustler.

“Nimeacha Kabisa madawa nina siku nne sijagusa toka nimejiunga na hii taasisi ya kuwaelimisha watu wanaohitaji kuachana na dawa za kulevya, nimejifunza kuvumilia arosto na matumaini yangu ni kuacha kabisa dawa kwani yameharibu maisha yangu kabisa". 


Alisema kwamba matumizi ya dawa za kulevya ni uharibifu wa pesa nyingi na kwamba amekaribisha dharau kwenye maisha yake.

Rapper huyo alisema endapo atafanikiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya atarudi katika kazi yake ya muziki, kwani anaamini ndiyo kazi pekee anayoiweza na mashabiki wake watakuwa wamemis kazi zake."Kundi la wanamuziki wa Nako 2 Nako na Weusi wananipa ushirikiano mzuri sana, wote wamefurahi kusikia nimeanza kuachana na dawa za kulevya".

akizungumzia wimbo wake wa sababu ni wewe, anasema kwamba,"niliimba mambo yote yaliyonitokea tangu nilipoanza kutumia dawa ya kulevya na jinsi yalivyo niharibia maisha yangu, matumaini yangu kwa vijana wanaotumia dawa watajifunza kutoka kwangu kuhusu madhara ya dawa za kulevya. 

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: