Kulingana na wenyeji hao, mwanamke huyo aliingia katika hoteli moja ambapo nyama hupikwa na kuuzwa na kuagiza kikombe cha supu.
Baada ya kuinywa supu hiyo, mwanamke huyo alimpatia muuzaji pesa lakini muuzaji huyo akawa hana pesa za kumpa salio lake. Ilimbidi muuzaji huyo atoke nje akataf
ute 'chenji’ na kumwacha mwanamke huyo hotelini peke yake.
Punde tu alipomwona muuzaji ametoka nje, mwanamke huyo alinyemelea mahali ambapo kulikuwa na nyama, akakichukua kipande kimoja na kukificha kwa 'baika’.
Akiyafanya haya yote, mwanamke huyo hakuwa na habari kwamba alikuwa akichunguliwa na wanawake ambao walikuwa wakiuza ndizi karibu na hoteli hiyo na ambao walimuarifu mwenyewe punde tu aliporejea.
Kizaazaa kilichozuka kiliwavutiwa watu wengi ambao walikuwa sokoni huku kila mtu akitaka kumpiga mwanamke huyo.
Polisi
Kwa bahati nzuri polisi kutoka kituo cha polisi cha Kibung’a walipashwa habari kuhusiana na kisa hicho na kufika mahali hapo kwa kasi. Mwanamke huyo aliokolewa kutoka kwa hasira za wenyeji.
Walimzuilia katika kituo cha polisi akingoja kufikishwa mahakamani ambako atashtakiwa kwa kosa la wizi.
Duru zinaarifu kuwa mwanamke huyo alianza kuiba baada ya kukatazwa kupika pombe haramu kufuatia msako mkali unaoendelea katika eneo hilo unaolenga kusitisha utengenezaji wa pombe haramu.
0 comments:
Post a Comment