MWANANCHI.
ALBERT MANGWEA.
P-FUN.
MKURUGENZI wa Studio ya Bongo Records, P-Funk, ‘Majani’ amewajia juu watu wanaotaka kujinufaisha na msiba wa Albert Mangwair, huku akiw
alaani vikali wanaotumia msiba huo kujipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa zisizo sahihi.

Majani alisema hayo kufutia kuenea kwa taarifa
kwenye mitandao ya kijamii zinazoonyesha picha ya msanii huyo akiwa
amepasuliwa tumbo na kukutwa na pipi za madawa ya kulevya wakati
akifanyiwa upasuaji.
Majani amesema kwamba taarifa kwamba alikutwa na pipi za madawa ya kulevya si za kweli kwa kuwa hakuna aliyethibitisha hilo.
“Kuna vitu vingi vya kuwafanya wawe maarufu,
lakini siyo kufanya vitu vya kudhalilisha maiti kwani ni maonyo ya dini
zote, ina maana watu wamemsahau Mungu kiasi hicho hadi kufanya mambo
yasiyoeleweka inashangaza sana, kibaya zaidi kuna baadhi ya watu wapo
huko kwa miaka mingi tunawaamini na wao wameingia kwenye mkumbo huo wa
kutoa habari zisizo na uhakika,”alisema Majani kwa hasira.
Majani alisisitiza kwamba kuna baadhi ya mambo
yanapaswa kuachiwa familia na endapo familia yake itahitaji msaada watoe
kadiri wanavyoweza.
Alisema hakuna sababu ya mtu au watu kujinufaisha
kwa kifo cha Mangwair ambaye alitumia nusu ya uhai wake kuitangaza nchi
kupitia muziki.
0 comments:
Post a Comment