Gari aina ya Mistubishi Fuso lenye namba ya usajili T 855 BZW likiwa limepata ajali baada ya kugongana uso kwa uso na scania katika eneo la Maseyu barabara kuu Dar es Salaam-Morogoro na kusababisha watu watano kufariki dun
ia iliyotokea majira ya juni mosi saa 1:45 usiku na kupelekea watu wawili kujeruhiwa mkoani Morogoro. Picha www.jumamtanda.blogspot.comWATU watano wamefariki dunia baada ya kutokea kwa ajali ilihusisha magari matatu katika eneo la Maseyu tarafa ya Mikese katika barabara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro katika tukio lililotokea majira ya saa 1:45 usiku wa Juni Mosi mkoani hapa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa BLOG WWW.JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM juu ya ajali hiyo Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao na Afisa Muuguzi wa zamu hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Yohana Sihaba walisema kuwa katika tukio hilo watu watano wamefariki dunia mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha majeruhi wawili kulazwa katika hospital ya mkoa.
Mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao akizungumza katika eneo la tukio alisema kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu aina ya Mistubishi Fuso lenye namba ya usajili T 855 BZW kugongana na Scania zenye namba ya usajili T 657 AFJ yaliyogongana uso kwa uso na wakati yakitaka kulipita scania nyingine yenye namba ya usajili na T 827 AJJ ambayo ilishindwa kupanda mlima na kuziba robotatu ya barabara na kupelekea watu watano kufariki dunia na majeruhi wawili.
Mbao alisema kuwa baada ya kufika katika eneo la tukio ilikutwa maiti moja na majeruhi wawili ambao walikimbizwa katika hopsitali ya mkoa kwa huduma na kuwataja majeruhi kuwa ni wafanyabiashara Exavery Haule (50) na Theo Mtega (28) ambao ni wakazi wa Njombe na Michael Mwenda (34) akiwa ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam na kubainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo bado jeshi la polisi linachunguza.
Naye Afisa Muunguzi wa zamu ya asubuhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro mara baada ya kufikishwa maiti hao na majeruhi, Yohana Sihaba alisema kuwa jana (juzi) majira ya saa 6 usiku Juni mosi walipokea jumla ya maiti wanne na majeruhi watatu waliofikishwa hospitalini hapo baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Sihaba alisema kuwa kati ya majeruhi hao watatu mmoja alifariki dunia hospitalini hapo wakati akipatiwa huduma ya kwanza na kueleza kuwa maiti wawili ndiyo waliotambuliwa na ndugu zao akiwemo maiti moja ya Theo Mtega.
Dereva wa Mistubishi Fuso ambaye anauguza majeraha ya ajali hiyo katika wodi namba mbili ya hospitali hiyo aliyejitambulisha kwa jina la, Trespholi Mlowe alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ilisababishwa na lori aina ya scani lenye namba ya usajili T 827 AJJ ambalo linadaiwa kushindwa kupanda mlima likitokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro na kufika eneo la kijiji cha Maseyu lilipata ajali na kuziba barabara.
Akieleza zaidi juu ya tukio hilo Mlowa alisema yeye alikuwa anatokea Morogoro kwenda Dar es Salaam na mara baada ya kufika eneo hilo aliona lori limeziba robotatu ya barabara hivyo kulazimika kupita pembembeni mwa barabara hiyo na mara baada ya kulipita lori hilo, lori lingine aina ya scania aligongana naye uso kwa uso na lori hilo na kupelekea uharibufu wa gari, majeruhi na maiti.
0 comments:
Post a Comment