Johannesburg.
Rais Jacob Zuma anaaminika kuwa na siri nzito ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela baada ya kufuta safari ya kwenda Maputo, Msumbiji alikokuwa akahudhurie mkutano wa marais wa nchi wanachama wa Ushirikiano wa Maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Rais Jacob Zuma anaaminika kuwa na siri nzito ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela baada ya kufuta safari ya kwenda Maputo, Msumbiji alikokuwa akahudhurie mkutano wa marais wa nchi wanachama wa Ushirikiano wa Maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Zuma alivunja safari hiyo baada ya kumtembelea
Mandela hospitalini na kumwona afya yake ikiwa imedhoofika, huku
akiendelea kusaidiwa kupum
ua kwa mashine.
ua kwa mashine.
Hatua ya Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma
kuahirisha safari yake ya Maputo, tayari kumeibua sintofahamu zaidi
kuhusu hatima ya afya ya Mandela.
Msemaji wa Rais Zuma, Mac Maharaj alisema kuendelea kuzorota kwa afya ya Mandela ni sababu ya kufutwa kwa safari hiyo.
Hata hivyo, Maharaj akizungumza kwa simu na gazeti
hili jana alikataa katakata kuzungumzia undani wa afya ya Mandela,
akasema jukumu hilo ni la familia yake na kwamba Ikulu inasaidia tu
katika masuala ya jumla yanayohusu afya ya kiongozi huyo.
Familia ya Mandela
Wakati familia ya aliyekuwa mpigania amani na
ubaguzi nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela wakipeleka mashine ya
kuchimbia kaburi katika makaburi ya kifamilia yaliyopo eneo la Qunu, kwa
mara ya kwanza, kiongozi huyo amefumbua macho na kurejewa na fahamu.
Taarifa iliyotolewa jana jioni na Ikulu ya Afrika
Kusini inasema Rais Zuma alimtembelea Mandela hospitalini mapema jana
ambako alipewa taarifa kwamba anaendelea vizuri. “Bado yuko mahututi
lakini imara,” ilisema taarifa ya Ikulu na kuongeza:
“Ana nafuu zaidi leo kuliko nilivyomwona jana (juzi) usiku. Timu ya madaktari inaendelea kumtibu.”
Hata hivyo taarifa hiyo ilimnukuu Rais Zuma
akilalamikia kile alichosema kuwa ni vyombo vya habari kutoheshimu
faragha ya mgonjwa.
Kauli hiyo ya Zuma ilitolewa muda mfupi tangu
binti yake Mandela alipovikosoa vyombo vya habari vya nje ya Afrika
Kusini, kwamba vinafanya kazi ya kuripoti tukio la ugonjwa wa Mandela
katika misingi ya ubaguzi wa rangi.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha SABC jana
mchana, Makaziwe alisema kitendo cha vyombo vya Magharibi kuweka kambi
nje ya Hospitali ya Medi Clinic alikolazwa baba yake ni kushindwa
kuheshimu desturi za Kiafrika.
CHANZO MWANANCHI.
CHANZO MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment