BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAPIGA MARUFUKU NDOA ZA JINSIA MOJA, UKINASWA TU ADHABU YAKE NI KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu.

Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.

Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi yakiwemo ya

ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa kunukuu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: