MTANZANIA.
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda.
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa
Ponda, amewatangazia Waislamu kwamba mihadhara iliyopigwa marufuku na
Serikali, itaendelea kufanyika kama kawaida na ataka
yeendelea kuikataza
watakabiliana naye kwa nguvu zote.
Sheikh Ponda aliyasema hayo
jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kwenye mamia ya Waislamu
waliokusanyika kwa ajili ya kongamano la kujadili mada mbalimbali,
ikiwamo uhuru wa Waislamu na haki zao na usalama wa watu, miradi na mali
zao.
“Tunatoa tamko kwa Waislamu, mihadhara iliyopigwa marufuku
itaendelea kufanyika kama kawaida, Waziri wa Mambo ya Ndani azingatie
kauli hiyo, hatuogopi ujinga, tunataka utaratibu ufuatwe, atakayekataza
mihadhara kufanyika tutakabiliana naye kwa nguvu zote,” alisema Ponda.
Alisema kwamba, Waislamu wamekuwa hawasikilizwi katika mambo mengi
wanayoomba kufanyiwa, lakini kwa upande wa maoni waliyotoa katika Katiba
Mpya wanategemea kuyaona yakiwamo.
“Endapo maoni ya Waislamu
hayataonekana katika Katiba mpya, tutaanzisha mtiti hadi kiama,
hatuogopi mtu, hapa tulipofikishwa hatukubali,”alisema Sheikh Ponda.
Alisema
kwamba, walipeleka mapendekezo serikalini, kwamba iundwe tume ili
waweze kupeleka madai yao, lakini hadi sasa tume hiyo haijaundwa.
“Kwa
hiyo, hatutarudi nyuma kudai haki zetu, tutatumia mazungumzo, kuandika
na kusema, kufanya mihadhara na makongamano, kufanya maandamano mchana
na hatimaye kufanya maandamano usiku na mchana.
“Pia, tunatarajia kufikisha mahakamani kesi nzito tatu kuhusu viongozi, sitazitaja kwa kuwa bado ni mapema mno,” alisema.
Naye
Sheikh Kondo Bungo, akizungumzia matukio yanayotokea nchini, alisema
Serikali inayo majibu ambayo yanatakiwa kuwekwa wazi ili wananchi
wayajue.
“Kuna dhana potofu imejengwa ili kuonyesha Waislamu ni
hatari, Zanzibar kumetokea mauaji ya Padri Mushi, makachero kibao
wamekwenda huko, baada ya siku mbili kanisa likachomwa, kweli kuna
mzanzibari gani mwenye kuweza kufanya tukio kama hilo katika mazingira
ambayo makachero wamejaa?
“Waislamu hatuna ugomvi na Wakrito,
chuki iliyopo ya kidini inapandikizwa na Serikali, kwa hiyo wakiristo
waungane na Waislam kuifanya Serikali iseme ukweli juu ya matukio
hayo,”alisema Kondo.
Akizungumzia umoja wa Waislamu, Sheikh
Nassoro Mohammed, alisema mkutano wao huo unathibitisha Waislamu ni
wamoja na hawana ugomvi na Wakrito isipokuwa ugomvi wao upo kwa
Serikali.
“Hatuna ugomvi na Wakristo bali ugomvi wetu upo kwa
Serikali kwani kuna haki zetu tunalalamikia hatupewi, mtu akidai haki
asipigwe badala yake asikilizwe na kueleweshwa, tunashangaa kuona watu
wakiijibia Serikali kuhusu madai yetu,” alisema Mohammed.
Akizungumzia
kufutwa kwa somo la dini kufanyiwa mtihani, Mwenyekiti wa Baraza la
Wakuu wa Shule, Hussein Pilly, alisema wanacholalamikia wao siyo kufutwa
kwa masomo ya dini bali kufutwa kwa mitihani ya masomo ya dini mwaka
huu.
“Hakuna aliyesema Serikali imefuta somo la dini shuleni,
somo la dini litaendelea kufundishwa, lakini halitafanyiwa mtihani,
hicho ndicho tunacholalamikia kwa sababu wanafunzi watakata tamaa
kulisoma,”alisema Pilly.
Kwa mujibu wa Pilly, kitendo cha somo la
dini kutofanyiwa mtihani, kitasababisha madhara kwa Waislamu na
Serikali kwa sababu somo hilo hadi kufikia hatua ya kukubaliwa kufanyiwa
mtihani, mijadala ilifanyika na wadau wakakubaliana ingawa sasa
mabadiliko yanafanyika bila wadau kushirikishwa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment