JAMBOLEO.Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipum
ba.
UJUMBE wa hatari unaotumwa kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) umenaswa na Serikali.
Tayari baadhi ya Watanzania wametumiwa ujumbe huo ambao unaeleza
namna ambayo umefika wakati wa mikoa ya Kusini kuwa Taifa huru ambalo
linaweza kujitegemea na kuhimizwa kutumwa kwa watu wengi zaidi ili
kufanikisha mkakati huo.
Akizungumza kuhusu ujumbe huo jana, mkoani hapa, Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema Serikali haitakubali kuona
kuna watu ambao hawaitakii mema Tanzania wanaotaka kuigawa na kwamba
tayari wanaendelea kufanya uchunguzi ili kuwadhibiti wanaotuma ujumbe
huo wenye lengo baya kwa Taifa.
“Kuna ujumbe mfupi unaotumwa katika simu za mkononi, ambapo
unazungumzia kuigawa Tanzania. Naamini kuna baadhi ya wananchi watakuwa
wameupata, lakini ni vema nikaurudia ili waufahamu unavyoeleza,” alisema
Dk. Nchimbi.
Alinukuu ujumbe huo ambao unasema hivi: Mtwara kuanzia jiwe la mzungu
Kilwa hadi Msimbati unapoishia Mto Ruvuma na Bahari ya Hindi Nanyumbu,
Liwale hadi Kinjumbi inatosha kuwa nchi kubwa kuliko Burundi, Rwanda,
Malawi Cape Verde, Botswana na zingine. Taifa letu litaiwa Tanzania ya
Kusini.
“Tumepeleke maombi ya kujitenga Umoja wa Mataifa tuwe nchi huru
Kusini kutoka zamani tuko nyuma ya pazia, kunja pazia liwalo na liwe.
Wao wao sisi kwa sisi, mbona Sudan wameweza kugawana nchi, tuma ujumbe
huu kwa watu wengi uwezavyo kwa watu wa Kusini,” ilisema sehemu ya
ujumbe ambao Dk. Nchimbi alikuwa akiinukuu.
Hata hivyo, aliwahakikishia Watanzania kuwa Serikali imejipanga
kikamilifu kuhakikisha watu wenye nia ya kuigawa nchi hii hawafanikiwi
na ipo tayari kutumia nguvu zake zote ili kukomesha watu wenye nia mbaya
na taifa hili.
Aliongeza kuwa kwa wale ambao watatumiwa ujumbe huo wanatakiwa kujibu
kwa kuandika ‘wrong number’ na kuongeza kuwa iwapo itatumwa meseji
inayozungumzia namna ya kuwagawa Watanzania kwa aina yoyote unatakiwa
kujibu hapo si mahala pale.
Dk. Nchimbi alisema pia iwapo watatokea watu ambao watafanya mikutano
ya hadhara, lakini inaonesha nia ya kuwagawa Watanzania, wasikubali
kusikiliza na badala yake waondoke eneo hilo kwani hiyo itamfanya huyo
anayehubiri kuigawa nchi kukosa watu wa kumsikiliza lakini kama haitoshi
bado wananchi wanatakiwa kumwambia kuwa hapo si mahala pake atatufute
mahali pa kusemea hayo mambo yake.
Kuhusu ujumbe ambao unaashiria kuigawa nchi, alisema Serikali
imejipanga na kutoa onyo ole wao ambao wanatumia simu za mkononi
kuhatarisha amani ya nchi kwani watasakwa kokote walipo kwa maslahi ya
taifa na kusisitiza wasijidanganye kwani hawataachwa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment