PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Kaimu mratibu wa mradi wa kilimo endelevu cha mseto wa mahindi na mikunde (SIMLESA) unaofadh
iriwa na Australia, Bashir Makoko akisoma risala wakati wa sherehe hizo.
Iranga akiendelea kutoa ufafanuzi kwa Ndiva.
Na Esther Mwimbula, Morogoro.
WATAFITI wa kilimo nchini wametakiwa kutumia tafiti zao kwa ajili ya kuinua sekta ya kilimo hususani kwa wakulima wadogo wanaotegemea kilimo kama shughuri kuu ya kiuchumi na kuendesha maisha yao ya kila siku.
Akizungumza na wakulima wa vijiji vya Msingisi, Ibuti, Tabu Hotel, Kwipipa, Luhwaji na Lubeho vilivyopo Wilayani Gairo Mkoani Morogoro, Kaimu mkuu wa wilaya ya hiyo Victor Ndiva alisema wakulima nchini bado wanahitaji msaada wa wataalamu wa kilimo katika kuinua uchumi wao kupitia sekta hiyo ya kilimo ili kuondokana na matatizo ya upungufu wa chakula na kuinua uchumi.
Ndiva aliwaeleza wakulima hao wadogo zaidi ya 500 ambao wanaotekeleza mradi wa matumizi ya kilimo hifadhi (SIMLESA) cha kilimo mseto cha mahindi na mbazi kuwa kundi hilo limekuwa likitegemea wataalamu kwaajili ya kuinua pato lao na serikali kwa ujumla.
Alisema kuwa endapo wakulima watapatiwa elimu kuhusiana na tabia ya nchi wataweza kulima kilimo chenye kuhifadhi ardhi kwa kutumia kilimo mseto ambacho kitawanufaisha na kuondoka na umasikini.
Kwaupande wake Mtafiti wa mbegu za kilimo kutoka katika kituo cha utafiti cha Chollima kilichopo dakawa mkoani Morogoro Geoge Iranga alisema alisema kuwa kujishughulisha na kilimo kutokana na mkoa wa Morogoro kuteuliwa kuwa ghala la chakula na kwenda sambamba na kauli mbiu ya kilimo kwanza ambayo imelenga kukitumia kama uti wa mgogo wa watanzania .
Alisema kuwa kuna baadhi ya wakulima wamekuwa wakitamani kulima kilimo hifadhi ambacho kina tumika kwa kulima bila kutifua badala yake wanatumia dawa ya maguu ili kuongeza tija katika uzalishaji kupitia kilimo hicho.
Naye Kaimu mratibu wa mradi wa kilimo endelevu cha mseto wa mahindi na mikunde (SIMLESA) unaofadhiriwa na Australia, Bashir Makoko alisema kuwa kilimo hicho kitawainua kiuchumi kwa kutumia eneo dogo na kupata mazao mengi ambapo awali walikata tamaa ya kuendelea na kilimo kutokana na kukosa mazao katika mashamba yao.
Makoko alisema kuwa mafunzo ya kilimo cha mseto cha mahindi na mikunde kilichotolewa kama darasa kwa wakulima wadogo wilayani.

Gairo Mkoani hapa kitawasaidia kujua mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuongeza tija ya uzalishaji katika sekta amabyo itasaidia familia zao kuondokana na tatizo la upungufu wa chakula kutokana na kutumia eneo dogo na kuvuna mazao mengi yatakayokisi mahitaji ya familia na kuinua pato la familia.
Aidha alisema kuwa taasisi hiyo ya utafiti ya SIMLESA inayojihusisha na utoaji wa elimu ya kilimo Mseto kilicholenga kwaajili ya kuinua maisha ya wakulima wadogo nchini imefanikiwa kutoa mafunzo ya kilimo Mseto kwa wakulima wanaoishi katika nchi za Ethiopi, Kenya, Malawi na Msumbiji kwaajili ya kuongeza tija katika sekta ya kilomo katika nchini hizo.
Hivyo aliwaomba watafiti na wadau mbalimbali wa kilimo kutumia njia mbadala ikiwemo kilimo mseto kwaajili ya kuwainua kiuchumi wakulima wadogo ambao wamekuwa wakitegemea kilimo kama ndiyo njia pekee ya kuwaingizia kipato na kujikwamua kimaisha.

0 comments:
Post a Comment