Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amewatahadharisha vijana kuwa wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu wasikubali kupewa rushwa ya kanga, fulana na fedha na mtu yeyote anayetaka kuingia madarakani.
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amewatahadharisha vijana kuwa wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu wasikubali kupewa rushwa ya kanga, fulana na fedha na mtu yeyote anayetaka kuingia madarakani.
Akizungumza jana alipokuwa kwenye bonanza la
michezo la kikundi cha Ukwamani Jogging kilich
opo Kawe, alisema vijana wawe makini katika kuchagua mtu mwenye uwezo wa kuongoza ambaye atajali masilahi ya wananchi wake siyo kwa masilahi yake binafsi.
opo Kawe, alisema vijana wawe makini katika kuchagua mtu mwenye uwezo wa kuongoza ambaye atajali masilahi ya wananchi wake siyo kwa masilahi yake binafsi.
“Najiuliza kama ninajiamini nataka kugombea Kawe
au Arusha au Sumbawanga kama ninafaa na wananchi wananiamini mimi
ninafaa na wananchi wananihitaji kwa nini niwachochee kwa kanga au fedha
ukiona hivyo huyo hawafai kuwaongoza,” alisema na kuongeza:
“Ukiona mtu anatoa kitu ili achaguliwe hafai kuwa kiongozi kwani uongozi ni mzigo,” alisema Sumaye.
Aliwashangaa watu wazima wanaochukua fedha na
kuweka mfukoni kisha wanapita mitaani huku wakisema fulani anafaa kwa
kuwa anatoa rushwa na fulani hafai kwa kuwa hatoi kitu chochote.
Sumaye alisema anayetoa fedha ili apewe kura huyo
hafai kuwa kiongozi kwa sababu atakuwa anawatumikia watu wake waliompa
fedha sio mwananchi ambaye alijitolea kumchagua kiongozi hiyo kwa
kumpigia kula halali ili aweze kusaidia kumtatulia kero mbalimbali
zinazomkabili.
Alisema kama kuna watu wanaumizwa kwa kuambiwa
wanapokea au kutoa rushwa huku akiwa anaendelea na kufanya hivyo aache
ili asiendelee kuumizwa na hilo.
Sumaye alisema nchi haiwezi kuwa na maendeleo kama
viongozi wataendelea kudidimiza nchi kwa rushwa,ufisadi na kuingiza
dawa za kulevya nchini.
Alisema viongozi wanaoleta dawa za kulevya kama ni
nzuri wangezitumia lakini hawazitumii matokeo yake wanaoathirika ni
vijana ambao wanategemewa kulijenga taifa hili.
“Hatuwezi kudidimiza jamii kwa kuwaletea dawa za
kulevya ili watoto wa wenzao waharibikiwe kwa nini wasiwape au kutumia
hao viongozi ili waathirike wao wenyewe?” alisema Sumaye.
CHANZO MWANANCHI
CHANZO MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment