BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA KITU KINACHODHANIWA KUWA NI BOMU MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI ZA UDIWANI CHADEMA SOWEPO JIJINI ARUSHA.

DAZANI YA WANACHANA, WAFUASI NA MASHABIKI WA CHADEMA KATIKA MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI ZA UDIWANI SOWETO JIJINI ARUSHA LEO.
WATU wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kamp
eni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hosp

itali ya Seliani na Mount Meru.

Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.

Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.

Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA.

ILANI: Baadhi ya picha zilizopachikwa hapo huenda zikagusa  hisia ya mtizamaji, tafadhali ikiwa huwezi kuvumilia kuona damu usibofye tarakimu zilizopo hapo chini kufungua picha zinazofuatia.

CHANZO http://mwanahabariuswazi.blogspot.com
 SEHEMU YA UMATI WA WAFUASI WA CHADEMA KATIKA MKUTANO HUO.WAHANGA WA TUKIO HILO
 
DAMU WANANCHI WAKIANGALIA DAMU ILIYOMWAGIKA KUTOKA KWA WAHANGA HAO.DAMU SAMBAMBA NA KANDAMBILI
GARI LIKIWA LIMEHARIBIWA
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: