PINDA ATAMANI LETECIA NYERERE ARUDI CCM
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA.
LETECIA NYERERE
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema
anatamani siku moja Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere (CHADEMA)
arudi Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pinda alitoa kauli hiyo jana jioni
wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Sumbawanga ng’ara kilichoandikwa na
Mbunge wa Viti Maalumu, Stella Manyanya (CCM), ambaye pia ni Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa.
Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika katika
hoteli ya Dodoma na kuhudhuriwa na Mawaziri, Man
aibu Mawaziri, viongozi kutoka Mkoa wa Rukwa, viongozi wengine wa Chama na Serikali.
aibu Mawaziri, viongozi kutoka Mkoa wa Rukwa, viongozi wengine wa Chama na Serikali.
Leticia Nyerere baada ya kuinuka ili
kutoa salamu zake ndipo Waziri Mkuu Pinda aliposema kuwa anatamani siku
moja Mbunge huyo wa Upinzani arudi CCM.
“Natamani siku moja urudi CCM,”
alisema Waziri Mkuu.
Hata hivyo baada ya Mbunge huyo kufika
mbele na kupewa kipaza sauti alisema ‘peoples power’ salamu ambayo
hutumiwa na chama cha Chadema, hali iliyofanya watu waliokuwa ukumbini
hapo kushindwa kujibu salamu hiyo na kubaki wakiangua kicheko.
Leticia alisema alikwenda pale kwa ajili
ya kumuunga mkono Manyanya ambaye ni mwanamke kiongozi jasiri, ambaye
mara nyingi amekuwa hasiti kuonesha ujasiri wake.
Alisema kuwa wabunge
wanatakiwa kuonesha ushirikiano katika masuala ya maendeleo badala ya
kuweka mbele itikadi za vyama.
“Tunapokuwa bungeni tunatakiwa tuwe wapinzani lakini tunapokuja katika suala la maendeleo tunatakiwa kuwa kitu kimoja,” alisema.
Leticia katika hafla hiyo aliongozana na
watoto wake wawili wa kike wanaosoma Maryland, Marekani na Waziri Mkuu
Mizengo Pinda alipowaona aliwataka watoto hao kwenda mbele ili
wasalimie.
“Hawa ni watoto wa Madaraka Nyerere, ni wajukuu wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,” alisema Waziri Mkuu.
Alipouliza watoto hao wamefanana na
nani, mmoja wa watoto hao alisema amefanana na bibi yake Maria Nyerere
huku mwingine akisema amefanana na baba na mama yake.
Pia akitoa salamu zake, mke wa Waziri
Mkuu Mama Tunu Pinda alimpongeza Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Manyanya kwa
juhudi anazofanya katika suala zima la kutunza mazingira.
Aliwataka wanawake wengine kuwa mstari
wa mbele katika kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali ikiwemo
kujitosa kuwania Urais mwaka 2015.
“Kwa nini mwanamke asishinde Urais wa mwaka 2015 wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini,” alisema Mama Pinda.

0 comments:
Post a Comment