HATIMAYE watanzania wamepata suluhisho la matatizo yao baada ya Tume
ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Jaji mstaafu
Joseph Warioba kutangaza mapendekezo ya katiba mpya iliyopendekezwa na
wananchi wenyewe.
Jaji Warioba ametangaza rasimu ya Katiba Mpya iliyojaa mabadiliko
makubwa huku ikikata kiu ya watanzani waliokuwa wakihoji masuala
mbalimbali ikiwemo suala la Serikali tatu, wabunge wa viti maalum pamoja
na nafasi ya Spika na Naibu wake.Akitangaza mapendekezo hayo ya katiba mpya katika Viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba alisema kwamba wamezingatia masuala mbalibali wakati wa kupitia na kuchambua maoni ya wananchi.
Kati ya mambo ambayo wananchi walikuwa wakiyapigia kelele ni suala la wabunge wa viti maalum ambayo Jaji Warioba alisema kwamba haitakuwepo katika katiba mpya badala yake nafsi hiyo itachukuliwa na kundi la watu wenye ulemavu ambao watakuwa wawili kutoka katika jimbo la uchaguzi ikiwa ni mwanaume na mwanamke. Chanzo http://www.habarimpya.com

0 comments:
Post a Comment