BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU WAWILI WATHIBITISHWA KUFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MLIPUKO WA BOMU WAKATI WA KAMPENI ZA UDIWANIA SOWETO ARUSHA.

MADAKTARI NA WAUGUZI WAKIWAPATIA HUDUMA ZA KITABIBU WATOTO WALIOKUWA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA JANA.Liberatus Sabas.

TUKIO la ugaidi iliyotokea katika mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesababisha vifo vya watu wawili na kujerugi watu 11,tukio hilo la kigaidi lilitokea wakati Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wakiwa katika hat
ua za mwisho za kufunga mkutano huo.

Akizungumza na Habarimpya.com Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema amepokea maiti moja ya mtoto na majeruhi 11, Wakati Mganga huyo akieleza kuwa amepokea maiti moja ya mtoto, Mwandishi wa Habarimpya.com alishuhudia zaidi ya majeruhi saba katika Hospitali ya Misheni ya Selian, huku pia ikidaiwa kwamba kuna maiti za watu watatu katika Hospitali hiyo.

Akizungumzia tukio hilo la ugaidi iliyotokea katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili mwanamke na mwanamume wamepoteza maisha, huku akidai kwamba bado wanafuatlia idadi ya majeruhi waliotawanywa katika Hospitali mbalimbali  mkoani humo.

Mashuhuda wa tukio walipozunguza na Mwandishi wa Habarimpya.com aliyekuwa katika mkutano huo jana walisema kwamba kuna mtu  alionekana akirusha kitu kilichodhaniwa kuwa ni bomu,kabla ajakamatwa Askari wa Jeshi la Pollisi waliokuwa wakilinda mkutano huo wakaanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya machozi na kupiga risasi za moto.

Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu wengi mkoani humo, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: