Frederic De Klerk (kulia) akifurahia jambo na Nelson Mandela mara baada ya kupitishwa kwa Katiba mpya ta nchi hiyo mwaka 1996. |
Kiongozi
wa mwisho wa Afrika Kusini ya ubaguzi wa rangi ambaye pia alitunukiwa
Tuzo ya Amani ya Nobel sambamba na Nelson Mandela kwa kusaidia
kuhitimisha utawala wa weupe wachache anatarajiwa kupachikiwa kifaa cha
kurekebisha mapigo ya moyo baada ya kuugua.
Rais wa zamani Frederic William de Klerk, mwenye umri wa miaka 77
alijihisi kizunguzungu baada ya kurejea nyumbani kutoka Ulaya Jumapili
iliyopita.
Alikuwa akisumbuliwa na matatizo kadhaa yanayof
anana na hayo ya kizunguzungu katika wiki za karibuni.
anana na hayo ya kizunguzungu katika wiki za karibuni.
Alitarajiwa kupachikiwa kifaa hicho cha kurekebisha mapigo ya moyo
jana kusaidia moyo wake kufanya kazi na alitarajiwa kubaki hospitalini
hapo usiku huo.
Hili limekuja huku Mandela, mwenye miaka 94, akitimiza siku yake ya
25 hospitalini jana baada ya mwanzoni kuwa amelazwa kwa kujirudia
maambukizi kwenye mapafu yake.
Tangu hapo, kumekuwa na hali ya sintofahamu nchini Afrika Kusini na
duniani kwa ujumla kwa mtu huyo ambaye alitumikia miaka 27 kama mfungwa
chini ya ubaguzi wa rangi na kisha kuibuka baadaye kujadiliana mwisho wa
utawala wa wabaguzi weupe kabla ya kuwa rais.
Akiwa rais, de Klerk alimwachia huru Mandela kutoka gerezani. de
Klerk na kiongozi huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi kisha wakaongoza
majadiliano ambayo yalihitimisha utawala wa wabaguzi weupe.
Yeye na mkewe, Elita hapo kabla walitangaza kuahirisha ziara ya
kikazi na mapumziko barani Ulaya sababu Mandela anaumwa mahututi.
Taasisi moja yenye makao makuu yake mjini Cape Town iliyopewa jina la
de Klerk ilisema rais huyo wa zamani alipatwa maradhi ya kizunguzungu
baada ya kurejea nyumbani Jumapili kutoka safari ya Ulaya, na kuonana na
daktari wake Jumatatu.
"Alikuwa na matatizo kama hayo katika wiki za hivi karibuni na
daktari wake alishauri upachikwaji haraka wa kifaa cha kurekebisha
mapigo ya moyo.
"Atapachikiwa kifaa cha kurekebisha mapigo ya moyo baadaye leo (jana)
na atakaa hospitalini hapo usiku mzima," taasisi hiyo ilisema katika
taarifa yake.
Rais wa Afrika Kusini alitoa taarifa jana akimtakia kiongozi huyo wa zamani kupona kwa haraka.
"Tunamtakia Rais huyo wa zamani afya njema katika kipindi hiki
kigumu. Wacha tumweke yeye na familia yake katika mawazo yetu na
maombi," alisema Jacob Zuma.
Jumamosi iliyopita taasisi hiyo ilitoa taarifa kwa niaba ya de Klerk
na mkewe, Elita, ikisema waliamua kuahirisha ziara ya kikazi na
mapumziko barani Ulaya sababu Mandela anaumwa sana, na kwamba walikuwa
wakimwombea kiongozi huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi aimarike afya
yake.
Mandela alipelekwa hospitali moja ya Pretoria Juni 8, mwaka huu
kutibiwa kile ambacho serikali ilisema wakati huo kurejea kwa maambukizi
kwenye mapafu.
Tangu hapo, hali yake imeendelea kuwa tete nchini Afrika Kusini na
duniani kote kwa mtu huyo aliyetumikia miaka 27 jela kabla ya kuja kuwa
Rais wa kwanza wa nchi hiyo katika uchaguzi huru mwaka 1994.
De Klerk, waziri wa zamani wa elimu ambaye alirejesha ubaguzi wa
shule, alikuwa muhimu katika kipindi kigumu cha mpito ambacho kiligeuka
na kuwa cha amani licha ya hofu ya kusambaa kwa mapigano ya kibaguzi.
Mwaka 1990, mwaka mmoja baada ya kuwa Rais wa Afrika Kusini,
akatangaza kukitambua chama cha African National Congress, kundi
lililopigwa marufuku ambalo liliongoza harakati za kupinga ubaguzi wa
rangi, na kuwezesha kuachiwa huru kwa Mandela.
Alitunukiwa Tuzo ya Noble sambamba na Mandela kwa juhudi zake za kimapinduzi na kwa haraka kuamua mwenyewe kuachia madaraka.
De Klerk baadaye alishika wadhifa wa makamu wa rais wakati wa awamu moja ya miaka mitano ya Mandela akiwa rais.
Tangu kustaafu kwake kutoka maisha ya siasa, amekuwa akisafiri kila
kona na kutoa mafundisho.
Taasisi yake inasema malengo yake ni kusaidia
mafukara na watoto wasiojiweza, kushiriki kutatua migogoro na kulinda
kikamilifu katiba ya Afrika Kusini, ambayo inasaidia kulinda haki za
binadamu.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari

Frederic De Klerk (kulia) akifurahia jambo na Nelson Mandela mara baada ya kupitishwa kwa Katiba mpya ta nchi hiyo mwaka 1996.
0 comments:
Post a Comment