Meneja
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vyakula vya
kufuturisha watoto yatima atika vitu vilivyopo mikoa ya Dar es salaam,
Mbeya, Arusha, Mwanza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na
meneja wa huduma za Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi.
Meneja
Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi akimkabidhi mwakilishi wa
Bakwata Ustadh Hassan Malangali vyakula vya kufuturisha katika mwezi
huu mtukufu wa Ramadhani vilivyotolewa kwa vituo vitatu vya watoto
yatima Dar es Salaam (hawapo pichani) vituo vitakavyofaidika zaidi ni
vya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha hafla ya makabidhiano
iliyofanyika katika ofisi za Airtel Morocco jijini Dar Es Salam .
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Airtel, Hawa Bayumi akimkabidhi tende Saida
Makope ambaye ni mwakilishi wa vituo vitatu vya watoto yatima Dar es
Salaam katika hafla ya makabidhiano ya vyakula vya kufuturisha katika
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani vilivyotolewa katika ofisi za Airtel, Dar
es Salaam jana. Anayeshuhudia ni mwakilishi wa Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (Bakwata), Ustaadh Hassan Malangali.
Na Mwandishi wetu.
KAMPUNI
za simu za mkononi za Airtel Tanzania kupitia Kitengo chake cha huduma
kwa Jamii wametoa msaada kwa vituo vitatu jijini Dar Es Salaam vya
watoto yatima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani vikifuatiwa na vituo
vingine katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kusaidia watoto
wanaolelewa kwenye vituo hivyo.
Msaada
huo umetolewa kwa lengo la kuwalenga watoto kutoka mikoa minne ambayo
ni Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa watoto hawa wanaohitaji
upendo hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Baadhi ya
vitu vilivyotolewa ni Mchele,Sukari, maharagwe,unga, mafuta ya
kupikia,maziwa, juice, majani ya chai na sabuni vyenye dhamani ya
shilingi milioni tano na nusu.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyoandaliwa
katika makao makuu ya Airtel jijini Dar Es Salaam, Meneja uhusiano wa
huduma kwa Jamii bi Hawa Bayumi alisema "kwa kutambua umuhimu wa Jamii
tunayofanya nayo biashara kampuni ya Airtel tumeamua turudishe kiasi cha
faida tunayopata kwa wananchi ili iwasaidie.
Akifafanua alisema kwa muda wa miaka 11 iliyopita tumeweza
kusaidia Jamii mbalimbali ya watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani na
bila kuacha nyanja za elimu, michezo kwa watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu na kukosa huduma mbalimbali za kijamii.
Kwa mwaka huu kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii
tutarudisha tulichokipata na tutaweza kufikia watoto zaidi ya 300 wa
mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha , Mwanza na Mbeya na mpaka sasa kwa
mwaka huu Airtel imegharamia zaidi ya shilingi millini 150 katika kukuza
kiwango cha elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania," alisema Bayumi.
Bayumi aliongeza kwa kusema kwamba Airtel inapenda kuwatakia
kheri na Baraka katika mwezi huu mtukufu na tangu kuanza kwa Mwezi
mtukufu wa Ramadhan, wateja wa Airtel wanaweza kufurahia huduma maalumu
ya Ramadhani kwa kutuma neno RAMADHANI kwenda namba 15322 kwa shilingi
153 tu kwa siku. Katika huduma hii mteja atapokea dua, nukuu za
qurani, mawaidha na taraweh salat moja kwa moja kwenye simu yake, kila siku.
Naye katibu mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila ambaye
alikuwa mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo makabidhiano ya chakula
imetoa fursa kwa waislam kutoka maeneo mbalimbali kukutana pamoja na
kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Aidha Lolila licha ya kuishukuru Airtel Tanzania kwa misaada
inayotoa kwa Jamii alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka
liungwe mkono na kuigwa na kampuni zingine hapa nchini.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment