Na
Juma Mtanda, Morogoro.
BONDIA
anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango vya masumbwi nchini katika
uzito wa kg 60, Cosmas Cheka (20) amemtaka mpinzani wake, Deo Njiku wote kutoka
mkoa wa Morogoro kusaini mkataba wa pamb
ano litakalowezesha mabondia hao
kutwangana kuwania mkanda wa PST unaoshikiliwa na Njiku katika mchezo
unaotarajia kufanyika Agosti 10 mwaka huu kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
Akizungumza
na gazeti hili mjini hapa Cheka alisema kuwa tayari amesaidi mkataba wa
kuzichapa na Deo Njiku katika mpambano la kuwania mkanda wa PST hivyo amemtaka
nay eye kusaini mkataba huo utaotoa nafasi ya kupigana Agosti 10 mwaka huu.
Cheka
anayeshikilia rekodi ya 274 katika viwango vya dunia vya ubora katika uzito wa
kg 60 ameeleza kuwa nia ya kuzichapa na Njiku ni kumtwanga na kutwaa mkanda
huo.
“Lengo
langu kwa sasa ni kuwa na mkanda wa PST ambao unashikiliwa na Njiku hivyo mimi
tayari nimesaini mkataba wa kuzichapa naye Agosti 10 hivyo ninasubiri nay eye
asaini ili niwe na uhakika kwa kumtwanga na kutwaa mkanda wa PST kwani najua
hawezi kunizuia kwa namna yoyote nisimpige”. Alisema Cheka.
Akieleza
sababu za kujigamba kumpiga Njiku, Cheka alisema sababu kubwa ni mazoezi
anayofanya chini ya makonda Abdallah Salehe (Komando) wakiwasaidiwa na Power
Iranda na Simon Ponela na kudai kuwa mpinzania wake ni mzuri kwa mabondia
wengine lakini sio nzuri kwa upande wake kwani suala la kumtwanga hilo halikwepeki.
Cheka
ambaye ni bingwa wa mkanda wa TPBO baada ya kutwanga bondia, Mussa Chipepeti
kutoka Songea, amelekeza nguvu katika pambano hilo ili kuweza kutwaa mkanda huo
wa PST huku akijiwekea malengo ya kufuata nyazo za kaka yake, Francis Cheka
(SMG) na kuwa na rekodi ya kumecheza mapambano 13 na kati ya mapambano hayo
akiwa ameshinda nane kwa pointi na kupoteza matatu kwa pointi na mawili kutoa sare.
0 comments:
Post a Comment