KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, familia ya Said Abdallah inayoishi
Buguruni jijini Dar es Salaam imelazimika kutokwa machozi upya baada ya
maiti ya mtoto Sophia Said (1) aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa malaria,
kuibwa na watu wasiojulikana na kaburi lake kuachwa wazi, Uwazi
limechimbua.
Kaburi alipozikwa mtoto Sophia Said likiwa wazi.
Uwazi lilifika eneo la tukio na kukuta umati, ikiwemo familia ya Said
ukitokwa machozi huku wakiliangalia kaburi hilo likiwa wazi.
Mbao na miti iliyotumika kwenye mazishi ya mtoto huyo vilikutwa pembeni ya kaburi.
Wakati watu wakiendelea kumwaga machozi huku wakiuliz
ana nini maana ya tukio hilo, Said ambaye ndiye baba mzazi wa marehemu alifika na kushuhudia maajabu hayo ambapo naye alishindwa kujizua na kuanza kulia.
ana nini maana ya tukio hilo, Said ambaye ndiye baba mzazi wa marehemu alifika na kushuhudia maajabu hayo ambapo naye alishindwa kujizua na kuanza kulia.
Baada ya hali kutulia kidogo, mwandishi wetu alihojiana na mfiwa huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nashindwa hata kuelezea vizuri kwani tangu nizaliwe sijawahi kuona
kaburi limefukuliwa, maiti haipo na isijulikane ilikopelekwa.
“Nikiwa kazini muda si mrefu uliopita nilipigiwa simu na shemeji yangu
Said Masoud ambaye anaishi maeneo haya, akaniambia kaburi lipo tupu na
haoni maiti ndani yake.
“Akasema mbaya zaidi, mbao na miti
iliyotumika siku ya mazishi viko pembeni kuashiria kwamba waliofanya
kitendo hiki ni watu waliokusudia.
“Niliishiwa nguvu, baadaye nilijikaza na kuja hapa. Ndiyo nimefika kama hivi na kukuta watu wengi nao wanashangaa.
“Nilipochungulia kaburi niliona ni kweli lilibaki tupu. Marehemu
alikuwa ni mtoto wangu wa kwanza, niliwazaa mapacha na kwa sasa amebaki
mwenzake aitwaye Salah.
‘Kinachonishangaza ni kwamba, marehemu tulimzika Juni 20 na kaburi limefukuliwa Julai 20, ina maana ni mwezi mmoja umepita.
“Sijajua kwa nini imetokea hivi! Mpaka sasa hakuna mtu ninayemshuku
kuhusika na tukio hili, inawezekana ni mambo ya kishirikina, nakwenda
kutoa taarifa polisi na kisha tutarudishia mchanga kaburini.
0 comments:
Post a Comment