KIONGOZI Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ), Askofu Dk.Alex Malasusa amesema nchi
haitakuwa na amani kwa kuongeza idadi ya polisi bali amani itapatikana kutokana na Watanzania kuheshimiana.
Askofu Malasusa aliyasema
hayo jana alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha
Faragha na maombi katika Kijiji cha Chasimba wilayani Bagam
oyo kitakachojengwa
kwa ushirikiano wa Usharika wa Dayosisi ya Kariakoo.
“Nchi haiwezi kuwa na amani kwa kuongeza idadi ya polisi njia pekee ni
kuheshimiana na kuheshimu madhehebu mengine ili kuendeleza amani,” alisema
Dk.Malasusa.
Aidha, alisema kituo hicho
kitajengwa kumbi za kisasa za mikutano, zahanati, chuo cha ufundi, maktaba na
nyumba ya faragha kwa ajili ya maombi na viwanja mbalimbali vya michezo.
Katika ibada hiyo mgeni
rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais Dk.Gharib Bilal, lakini aliwakilishwa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dk.Theresia Huvisa.
Akizungumza kwa niaba ya
Makamu wa Rais Dk.Huvisa alisema serikali itashirikiana na taasisi mbalimbali
zikiwamo za kidini kusaidia kuendeleza maendeleo.
Ofisi yake ilichangia
Shilingi milioni mbili katika harambee iliyofanyika kwa lengo la kupata milioni
200 kuendeleza ujenzi huo.
Katika harambee hiyo
iliyoshirikisha viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi Mchungaji
Daniel Thabita kutoka Botswana alichangia Sh.milioni 1.5.
0 comments:
Post a Comment