Hivi
karibuni mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa akifuturu na hawara
yake, Penniel Mungilwa ‘Penny’, kitendo ambacho kimewashangaza wengi na
baadhi kufikia hatua ya kumponda kuwa anakwenda kinyume na Uislam.
Tukio hilo lilijiri nyumbani kwa Diamond maeneo ya Sinza- Mori jijini
Dar ambapo mbali na mastaa hao, pia walikuwepo waumini wengine wa dini
hiyo walioalikwa katika chakula hicho kitakatifu.
Wakizungumza
kwa hisia mara baada ya kumuona Penny ambaye ni demu wa Diamond akiwa
eneo hilo, baadhi ya waumini walisema walishangazwa na uwepo wake kwani
sheria ya dini ya Kiislam hairuhusu kuwa karibu na kimada hasa katika
kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Walisema, Diamond
hatakiwi kuwa karibu na Penny si kwa kipindi hiki tu bali hata baada,
mpaka pale ambapo atatoa mahari na kuozeshwa kwa kufuata misingi ya dini
ya Kiislam.
“Huyu
kijana kafanya jambo zuri la kuwafuturisha wenzake ila amekosea
kumualika yule mwanamke wake, yule kwake ni kimada na kwa sheria za dini
yetu huruhusiwi kabisa kumkaribia, sasa ona wanafuturu pamoja na
wanashikanashikana, ile siyo sawa,” alisema muumini mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Swaleh alisema: “Diamond anatakiwa aambiwe kuwa anafanya makosa sana kuwa karibu na yule Penny.
“Kihalali
kwanza anatakiwa amsilimishe kisha amlipie mahari ndipo amuoe lakini
kinyume na hapo atakuwa anaishi na hawara na kuwa naye karibu ni
kujichumia dhambi anazoweza kuziepuka.”
Mashehe nao wacharuka
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, baadhi ya mashehe wenye heshima kubwa Tanzania nao
walionesha kukerwa na kitendo alichokifanya Diamond na kusema kinakiuka
maadili ya dini yao. Walisema, mwanamke ambaye hajaolewa anayeishi au
kuwa karibu na mwanaume na wakati mwingine kuzini, huyo ni kimada na
hana nafasi kwenye Uislam.
Shehe Khamisi Mataka
Huyu ni
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mashehe na Wanazuoni Tanzania anasema: “Lengo
la swaumu ni kumfanya mtu kuwa Mchamungu na Mchamungu ni yule anayefanya
yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na kuacha aliyokatazwa. “Katika
Uislam kuwa na hawara inakatazwa, si kwa kipindi hiki tu cha Mwezi
Mtukufu bali hata baada. Kwa hiyo kufuturu na hawara ni kinyume na
Uislam na unapata dhambi.”
Maalim Hassan Yahya
Ni
Mnajimu maarufu nchini. Yeye anasema kuwa, hawara hakubaliki kidini
hivyo hatakiwi kupika futari wala kuwa naye karibu kwa namna yoyote,
kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za funga na maadili ya
Uislam.
Shekh Alhad Musa Salum
Huyu ni
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kuhusiana na hili la Diamond la
kufuturu na Penny anasema kuwa, uhawara hauruhusiwi katika Uislam na
wanaoendekeza hilo waache mara moja ili waweze kupata radhi za Mwenyezi
Mungu.
Shehe
Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban Simba hivi karibuni aliwasihi Waislam
kutimiza nguzo hiyo muhimu ya Uislam na kuwataka wahakikishe wanafuata
sheria na taratibu zilizowekwa ili waweze kufikia lengo la kufunga.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment