AAPA KUMPA KICHAPO DADA SINTAH POPOTE ATAKAPO KUTANA NAYE KISA....
MWIGIZAJI
wa kike wa filamu na muziki Bongo Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemtangazia
hali ya hatari msanii mwenzake wa filamu na mtangazaji wa televisheni
Christina John ‘ Sintah’ kuwa popote atakapomkuta lazima amchape kwa
kipigo ambacho hatasahau katika maisha yake, Shilole kaongea hayo
kufuatia kuandikwa na mwanadada huyo katika mtandao wake akimbeza kwa kejeli. .
“Ni
kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu
anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina
uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda
kufanya show Marekeni! Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye
nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi,”aliongea kwa hasira Shilole.
.
.
Katika
mtandao wake Sintah aliandika kwa kusema Shilole ni sawa na mtu
anayeota ndoto za mchana, na kumkejeli kwa kusema kuwa aendelee kuota
anaweza baadae kurudi katika hali yake, sehemu ya maneno yanayomkera
Shilole ni haya
“Shilole
bwana hii week katujia na kali kuliko eti ameongea na Benny Medina
(Jlo’s Manager) ili aweze kufanya collabo na my sister, heee yes
inawezekana maana hakuna lisilowezekana chini ya jua lakini swali ni??
wataimbaje?? yule dada yake na mie ni RnB na music wa Shilole bado
sijaujua ni chakacha ama nini sasa naomba msaada kwenye tuta wadau wa
music, hili linauwezekano??,”
“ Chakacha na RnB?? Kwa sababu Shilole nyimbo zake sawa na Snura wa majanga, kidogo Linah angeniambia ana collabo na my sisy ningeelewa sasa Shilole?? Ndoto za mchana ila si vibaya kuota maana ukishtuka unarudi ktk reality,”

Shilole
anasema kuwa hajawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama Sintah,
anajifanya anambabaikia Jlo wakati hata hajulikani, ameshangaa watu wa
Bongo kuwa na tabia ya kudharau muziki wa nyumbani na kubabaikia muziki
wa Marekani wakati wenyewe hawana muda muziki wa hapa Bongo, anamchukia
Sintah kwa kuongea kitu asichojua na kumponda yeye na Snura.
“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-lo kuimba naye lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu alikubali kufanya kazi na mimi, ilitakiwa nionane naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,” anasema Shilole.

anasema Mungu ni mkubwa hata kama kuna mtu anayemchukia kwa mafanikio
yake bado Mungu ana nafasi kubwa kuwazima watu wenye roho mbaya wivu
kama Sintah ambaye anaonekana yupo tayari kwa ajili ya kuwaombea
matatizo watu wanaojituma kwa ajili ya kuendesha maisha yao
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment