MKAKATI wa kuwaengua vigogo wanaotajwa kung’ang’ania kugombea nafasi
ya Urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 sasa umebainika, MTANZANIA
Jumapili linaripoti.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina uliofanywa
na gazeti hili, mkakati huo ambao umelenga kuwang’oa viongozi hao,
unadaiwa kutekelezwa na baadhi ya wanas
iasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kupitia Rasimu ya Katiba Mpya, iliyotolewa hivi karibuni na Tume
ya Mabadiliko ya Katiba.
Imeelezwa
kuwa kupitia Rasimu hiyo ya Katiba Mpya, kuna vipengele vilivyopenyezwa
kwa nia ya kuwabana watu fulani fulani ndani na nje ya CCM ambao
wanatajwa kuusaka ukuu wa dola mwaka 2015 na chama hicho hakitaki kuona
wanakuwa kikwazo dhidi yake.
Mtoa habari wetu ndani ya CCM alilidokeza gazeti hili kuwa vipengele
hivyo ambavyo vimewekwa kama mtego, ni vile vinavyotaja sifa za mgombea
Urais na mgombea Ubunge.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizotufikia, kutokana na hilo, baadhi ya wanasiasa
ndani ya CCM kwa makusudi wameamua kuufanya mjadala kuhusu serikali tatu
kuwa mkali, ili kuzuia mjadala mpana katika masuala mengine.
Kipengele
ambacho kama kikiachwa bila kufanyiwa marekebisho kinaweza kuwabana
wanasiasa wengi ndani na nje ya CCM wanaotajwa kuwania Urais 2015 ni
pamoja na kile cha Sura ya Saba, ambacho kinazungumzia Serikali ya
Jamhuri ya Muungano kuhusu Serikali, Rais na Makamu wa Rais, katika
sehemu ya kwanza C kwenye kipengele cha 75 (E) kinachozungumzia sifa za
Rais kimeeleza kuwa mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya
madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa: anazo sifa za kumwezesha
kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hiyo.
Wakati ikiwa hivyo katika sifa za kuwania nafasi ya Rais, kwenye
Rasimu hiyohiyo kipengele cha sifa za kuwania nafasi ya Ubunge kilichopo
katika sura ya tisa, sehemu ya pili (A) inayozungumzia kuhusu uchaguzi
wa wabunge, katika kipengele cha (2a) kimeeleza kuwa mtu hatakuwa na
sifa za kugombea/ kuchaguliwa kuwa Mbunge ikiwa mtu huyo aliwahi kuwa
Mbunge kwa vipindi vitatu vya miaka mitano.
Kutokana na hilo, ni
wazi kuwa viongozi au vigogo waliowahi kuwa wabunge kwa vipindi zaidi ya
vitatu vya miaka mitano hawatakuwa na sifa za kugombea Urais kwa sababu
tayari kipengele cha sifa za kuwania Urais kimetaja kuzingatia sifa za
mgombea ubunge.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti
hili, umebaini kuwa vigogo karibu wote ndani na nje ya CCM wanaotajwa
kutaka kuwania nafasi ya Urais watakuwa wamepoteza sifa za kuwania
nafasi hiyo endapo kipengele hicho kitaachwa bila kufanyiwa mabadiliko.
Vigogo
hao wanaotajwa kutoka CCM ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta,
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli,
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Wengine ni Waziri wa
Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, Januari Makamba, wakati kutoka Chadema ni Mbunge wa Hai,
Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbroad Slaa na Zitto
Kabwe.
Watakaokuwa wametupwa nje
Kulingana na sifa
zinazotajwa kwenye kipengele hicho, viongozi wanaotajwa kutaka kuwania
nafasi hiyo lakini watakuwa wamegonga mwamba ni pamoja na wafuatao;
Edward
Lowasa ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa muda wa miaka miwili na hadi
sasa ni Mbunge wa Monduli kupitia CCM, ameshika nafasi hiyo kwa vipindi
vitano vya miaka 25 kuanzia mwaka 1990 hadi sasa, moja kwa moja atakuwa
amepoteza sifa ya kuwania Urais, kwani tayari amezidi vipindi vitatu
vya kuwa mbunge.
Samuel Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo
Mashariki (CCM), ameshika nafasi hiyo kwa vipindi sita kwa muda wa miaka
30, kuanzia mwaka 1975 hadi 1995 na 2005 hadi sasa, naye pia atakuwa
amepoteza sifa.
Dk. John Magufuli, ambaye ni Mbunge wa Chato
(CCM) kwa vipindi vinne vya miaka 20 kuanzia mwaka 1995 hadi 2015, naye
atakuwa ameshapoteza sifa, kwani amezidi vipindi vitatu.
Bernard
Membe, ambaye pia ni Mbunge wa Mtama (CCM) naye atakuwa ametupwa nje,
kwani hadi sasa ameshika nafasi hiyo ya Ubunge kwa vipindi vitatu vya
miaka 15 kuanzia mwaka 2000 hadi 2015.
Dk. Willborad Slaa,
atakuwa ametupwa nje ya ulingo kwani amewahi kutumikia vipindi vitatu
vya Ubunge kunzia 1995 hadi 2010 katika Jimbo la Karatu kwa kupitia
Chadema.
Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
atakuwa ametimiza sharti la kuwa mbunge kwa vipindi viwili, lakini
atagonga mwamba katika sharti la umri, kwani atakuwa hajatimiza umri wa
miaka 40 kama rasimu ilivyoendelea kupendekeza, badala yake atakuwa na
umri wa miaka 39.
Waliosafishiwa njia
Dk. Harrison Mwakyembe,
ambaye ni Mbunge wa Kyela (CCM) ameshika nafasi hiyo vipindi viwili vya
miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2010.
Dk. Emmanuel Nchimbi
ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini (CCM) ametumikia nafasi hiyo kwa
kipindi kimoja cha ubunge wa jimbo kuanzia mwaka 2010 hadi sasa.
Januari
Makamba, ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) amedumu kwa kipindi kimoja
kuanzia mwaka 2010 hadi sasa hivyo atakuwa na sifa za kuwania urais.
Freeman
Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na Mbunge wa Hai, naye
atakuwa na sifa ya kuwania nafasi hiyo, kwani atakuwa ametumikia nafasi
hiyo kwa vipindi viwili kwa miaka 10 kuanzia 2000 hadi 2005 na 2010 hadi
sasa.
Suala la Urais limezua mjadala mkubwa ndani na nje ya CCM,
baadhi wakikomoana kuhakikisha mwingine hapiti kwenye nafasi hiyo. CCM
ndicho kinachoonekana kuathirika zaidi, kwani jambo hilo tayari
limesababisha makundi yanayosigana.
CHANZO MTANZANIA
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment