BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HII ILIKUWA SAHIHI KWA FBI KUKAGUA OFISI YA KOVA NA MBWA ?.


File:FBI dog Dolce.jpg
KAMA OFISI ZA WANAUSALAMA ZINAKAGULIWA KWA NAMNA HIYO WATU WENGINE HALI IMEKUWAJE !.

OFISA mmoja wa Usalama wa Marekani (FBI), hivi karibu wakati wa ziara ya Rais Barack Obama akiwa na mbwa aliingia Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kufanya ukaguzi.

Tukio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya msafara wa magari ya Marekani kupita yakitokea Ikulu kwenda Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kumlaki Rais Barack Obama.

Polisi ambaye hakutaka kutajwa alisema ofisa huyo  aliingia na mbwa hadi maeneo ya mapokezi, lakini muda mfupi walitoka.

“Walikwenda moja kwa moja map
okezi wakafanya ukaguzi,  kisha wakatoka nje ya jengo na kama hiyo haitoshi, ofisa huyo akiwa na mbwa alikwenda sehemu ya kuegesha magari yenye kesi na yale ya kawaida na kuanza kufanya ukaguzi, baada ya hapo waliondoka,” alisema polisi huyo na kuongeza.

“Licha ya mimi kutokuwa na  cheo pale, lakini hili la kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi ndiyo tunaaminika kwa usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo Kikuu.”

Hata hivyo, usalama kwenye vituo vingi ikiwamo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juliusu Nyerere, vilikuwa chini ya usimamizi na uangalizi wa makachero wa Marekani.
CHANZO MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: