Shujaa wa leo; Kipa wa URA, Yassin Mugabi akiwa amejibweteka chini huku Jerry Tegete akikimbia kushangilia bao la kusawazisha aliloifungia Yanga jioni hii Uwanja wa Taifa. |
ANGALAU Yanga wanaweza kujisifu tayari wana timu kuliko wapinzai wao, Simba SC. Baada ya jana URA ya Uganda kuifunga Simba SC mabao 2-1, leo imekwaa kisiki kufuatia kulazimishwa sare ya 2-2 na mabingwa wa Bara, Yanga SC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Lakini
haikuwa sare nyepesi, kwani mabingwa wa Tanzania Bara walilazimika
kuhaha kusaka mabao ya kusawazisha hadi walipojitoa uwanjani salama
dakika ya 90 kwa bao la Jerry Tegete.
Katika
mchezo huo, uliochezeshwa na refa Kennedy Mapunda aliyesaidiwa na Iddi
Maganga na Othman Othman, hadi mapumziko URA tayari walikuwa mbele mkwa
bao 1-0.
Mkombozi; Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete akikabiliana na mabeki wa URA. Tegete leo ameinusuru Yanga kuzama mbele ya URA kwa kufunga bao la kusawazisha dakika za lala salama. |
Bao hilo lilifungwa dakika ya 42 na Litumba Yayo, ambaye jana Watoza Kodi hao wa Uganda wakiilaza Simba SC 2-1, alifunga mabao yote.
Kipindi cha kwanza URA ndio waliotawala mchezo kwa kucheza kwa kasi nzuri, uelewano mzuri na kushambulia kwa nguvu, wakati Yanga SC walionekana kukosa mipango.
Kipindi cha pili, URA walianza tena vyema na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 61, mfungaji Yayo tena akiweka rekodi ya kufunga mabao manne Taifa ndani ya siku mbili.
Kocha Mholanzi, Ernie Brandts alilazimika kufanya mabadiliko baada ya bao hilo, akiwaingiza Haruna Niyonzima kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi wingi ya kulia, Bakari Masoud kuchukua nafasi ya Hamisi Thabit na Abdallah Mnguli ‘Messi’ kuchukua nafasi ya Shaaban Kondo.
Mabadiliko hayo yaliisaidia Yanga SC ambayo iliongeza kasi ya mashambulizi na kufanikiwa kuchomoa mabao yote, moja baada ya lingine.
Mrundi Didier Kavumbangu alianza dakika ya 66 akiunganisha krosi ya beki Juma Abdul kabla ya Tegete kusawazisha dakika ya 90 baada ya kuwazidi nguvu na maarifa kipa wa URA, Yassin Mugabi na mabeki wawili.
Alivyofunga; Tegete akikabiliana na mabeki wa URA na kipa wao kabla ya kufunga |
Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Ibrahim Job, Rajab Zahir 14, Salim Telela 2, Said Bahanuzi/Niyo, Hamisi Thabit 28/Bakari Masoud, Jerry Tegete, Didier Kavumbangu na Shaaban Kondo18/Abdallah Mguli.
0 comments:
Post a Comment