Mshambuliaji wa timu ya soka ya Gereji SC, Meshack Seleman kushoto akipimana ubavu na mlinzi wa Black People, Jobeki Seleman kulia wakati wa ligi ya Nanenane Cup 2013 katika mchezo wa pili mtoano ambapo mchezo huo Gereji walisonga mbele kwa jumla ya bao 1-0 kufuatia kutoa sare tasa ya 0-0 katika mashinda yanayoendelea kwenye uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Gereji SC, Meshack Seleman a.k.a Mbuyu Twite.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU ya soka ya Gereji FC imekuwa ya kwanza kutinga hatua ya 16 bora mtoano katika mashindano ya ligi ya Nanenane Cup 2013 kufuatia kuiondoa Black People kwa jumla ya bao 1-0 kwenye uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa mzunguko wa pili dhidi ya Black People uwanja wa Sabasaba mjini hapa, Meneja wa timu ya Gereji, Yassin mwange alisema kuwa timu yao imefanik
iwa kusonga mbele kwa faida ya bao moja la mchezo wa kwanza maboa waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mwange maarufu kama Staff one alisema kuwa sare tasa ya 0-0 ya mchezo wa pili imeisaidia kuitoa Black People mashindanoni na uongozi mzima upo katika mkakati wa nguvu katika mchezo wa hatua ya 16 bora mtoano ili na mchezo huo kuweza kushinda na kutinga hatua ya timu nane bora za kusaka ubingwa wa ligi ya Nanenane CUP 2013 na kupiga mahesabu ya kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.
“Hii timu tunataka kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza kuundwa na kutwaa mataji na sasa hivi historia hiyo kuiweka kwa kutwaa makombe mawili likiwemo la TIKA CUP 2013 na mashindano haya ya ligi ya Nanenane Cup 2013 kwani timu yetu ndiyo imeundwa mwaka huu na tunataka mpaka mwaka unaishi tuwe na vikombe zaidi ya vitatu katika ligi tutakayoshiriki na hilo linawezekana kwa sababu tumesajili wachezaji wazuri wenye vipaji vya soka”. Alisema Mwange.
Licha ya timu ya Gereji kuwa ya kwanza kutinga hatua ya 16 bora mtoano kabla ya kucheza ligi ya timu nane na kupata bingwa, timu nyingine zenye nafasi ya kutinga hatua hiyo ni pamoja na Black Viba iliyopata ushindi katika mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Chipolopolo kwa kuilaza bao 4-3 huku Sabasa nayo ikijiweka nafasi ya kusonga mbele kwa ushindi wa mchezo wa awali wa bao 2-1 na Welazi FC.
Nyingine ni pamoja na Terminal iliyoibuka na ushindi wa bao 2-1 kwa kuitandika Nato FC, Kaizer Chief iliilaza Mazimbu Market bao 3-1, Dakawa Rangi ikiizaba Chamwing Rangers bao 2-1 na Jamaica kwa kuitambia Spazi FC bao 2-1.
Hiace Termina iliikung’uta Road kwa bao 2-1 wakati michezo ya timu ya Uruguary dhidi ya Bigwa na Moro Kids na Mgulasi FC zenyewe zilishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya bao 1-1 kila mchezo ambapo mshindi wa kwanza anatarajiwa kuondoka na kitiza cha sh700,000 huku nafasi ya pili ni sh350,000 na mshindi wa tatu akiambulia sh150,000.
0 comments:
Post a Comment